WOKOVU KWANZA *sehemu ya nne *

mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla
Ni lazima ifike wakati tutambue kwamba maisha ambayo Bwana Mungu ameyakusudia kwetu sisi,ni maisha ya WOKOVU na si mengineyo.
Bwana Mungu anatutizamia tuishi humo,na si pengine. Anatutizamia tuishi katika ushindi dhidi ya dhambi,tena ushindi dhidi ya kila aina ya nguvu ya giza maana Yeye mwenyewe alishatushindia yote pale msalabani.
Katika fundisho hili "WOKOVU KWANZA" tumemuangalia mtu mmoja tu,aitwae Zakayo, kama mtu aliyechagua fungu lililo jema machoni pa Bwana. Wala hatukuwaangalia watu wengine wengi walioamua kuacha vyote na kumuelekea BWANA MUNGU katika njia ya maisha ya WOKOVU,maana wapo wengi tu,ila hata kwa hao wengi ambao hatukuwazungumzia pia yapo mengi ya kujifunza,lakini kwa mfano mmoja tu wa Zakayo unatosha kabisa.( Luka 19:1-10)
Zakayo anatupa fundisho kubwa sana,akituonesha kwamba maisha ya dhambi sio dili,bali dili ni maisha ya kuishi ndani ya Yesu Kristo,kuokoka.
Yesu Kristo anapoingia kwa mtu,mtu huyo gafla hugeuka kutoka katika njia ya uharibifu/ upotevuni,na kuingia uzimani kwa maana mtu uamua kuacha vyote vya dhambi kwa kuvifuata vyenye utakatifu tena pasipo hata kushurutishwa.

" Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. " Luka 19:8
Zakayo hakuambiwa avitoe vyote alivyo nyang'anya,bali kulikuwa na nguvu ya Mungu iliyomsukuma hata yeye kuviachilia vyote kwa ajili ya Bwana.
Na hivi ndivyo hali ilivyo,Yesu anapoingia ndani yetu huwa tunajikuta tukiviacha vitu au mambo yote ya awali yenye kusababisha dhambi hata kama bado tunayapenda.

Mfano:
Wengine tulikuwa walevi,wazinzi,wezi N.k Lakini tulipookoka na KUDUMU katika maisha ya wokovu,taratibu mambo hayo yote yalianza kuondoka ndani mwetu,moja baada ya jingine pasipo hata kushurutishwa.

Maisha yetu yanafananishwa na mfano huu:
Chukulia soda ya Coca cola,kisha uimimine katika glass,ile glass itaonekana ni nyeusi sababu ya uwepo wa soda. Then,ukianza kumimina maji ndani ya glass yenye ile soda ya Coca cola,utaona taratibu weusi wa ile soda ukipotea. Na ukizidi sana kuweka maji katika hiyo glass utaona weusi ukizidi sana kuondoka na kuukaribisha weupe,na hatimae maji ya weupe yatatawala.

Ndivyo tulivyo sisi.
Pindi tunapookoka,wengi tunakuwa hatujaacha vijitabia vya dhambi ingawa tumeokoka. Utakuta kweli tupo nyumbani mwa Bwana na kuitwa walokole,lakini bado tuna vijitabia vya uzinzi ndani yetu,
Bado tuna vijitabia vya ulevi ndani yetu,
Bado tuna vijitabia vya kusengenya ndani yetu,
Bado tuna vijiroho vya chuki ndani yetu,N.k

Hivyo tunakuwa ni weusi ndani ya glass,Lakini kadri tunapoendelea kudumu ndani ya nyumba ya Bwana kwa KULISIKIA NENO LA KRISTO,taratibu weusi wa dhambi hutoweka na hatimaye,tu safi sasa.
Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe sana...

WOKOVU KWANZA yatosha!
Hakuna mtu aliye ndani ya wokovu kisha akajuta kuwepo humo. Au kwa lugha ya urahisi kabisa niseme hivi;
Hakuna majuto ndani ya wokovu,maana Mungu U pande wetu;
" Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu. " Zab.118 :6-8

Biblia inaposema " HERI" ina maana "BARAKA" yaani amebarikiwa yule anayemkimbilia Bwana " Heri kumkimbilia Bwana..."
Kwa lugha nyingine,mbaraka wa Bwana umefichwa ndani ya kuyafanya mapenzi yake,nje ya hapo hakuna mbaraka.

Haleluya...
Sema;
AMEN...

Tunasoma tena habari ya Zakayo,imeandikwa;
" Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. " Luka 19:10

Ujio wa Bwana Yesu ulikuwa kwa ajili yako pamoja na mimi,watu tuliokuwa dhambini,lakini si hivyo tu. Bali zaidi sana alikuja kutafuta kile kilichopotea. Kulikuwa ni kitu cha zaidi kilichopotea,nacho ni;
Ushirika wa Roho mtakatifu.

Ushirikia wa Roho mtakatifu ni bond/Conection au ni muunganiko wa Roho mtakatifu ndani ya roho ya Adamu katika MWILI WA UTAKATIFU.
Ikumbukwe kuwa;
Mwanadamu wa kwanza alikuwa na mwili wa utukufu,ambao haukuwa na dhambi yoyote.roho ya mwanadamu iliweza kuwasiliana moja kwa moja na Mungu Baba,biblia inasema Mungu alikuwa akishuka wakati wa jua kupunga,huu ni utukufu,imeandikwa;

" Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga;... " Mwanzo 3:8a
Bwana Mungu alikuwa akishuka,akizungumza na Adamu,mwenye mwili wa utukufu.
Sasa angalia;
Dhambi ilipoingia tu,ushirika wa Roho mtakatifu na mwanadamu ukapotea,ndiposa BWANA MUNGU akamtuma Bwana Yesu aje kurejesha ushirika wa Roho mtakatifu uliopotea kwa mwanadamu sababu ya dhambi isiyotubiwa.

Kwa lugha nyingine,lugha ya wepesi kabisa ninaweza kulinganisha na mfano huu;
Chukulia mawasiliano kwa njia ya simu. Mtu anayetumia simu huweza kuwasiliana na mwenziye mwenye simu kwa sababu kuna kitu kinachowaunganisha hawa wawili wenye simu,kitu hicho ni NETWORK.
Endapo network ikiondoka basi watu hawa wawili hawawezi kuwasiliana,wala hawawezi kuonana,kwa sababu network imepotea.

Ushirika wa Roho mtakatifu ulikuwa ni kama network kati ya Mungu na mwanadamu,ndio maana baada ya ushirika huu kuondoka,tunaona Mungu akishindwa kumuona Adamu mahali alipopaswa kuwa,tunasoma;
" Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? " Mwanzo 3:9
Si kama Mungu alikuwa hajui Adamu yupo wapi,alijua. Lakini alipomuona sipo alipomkusudia kumuona,sababu ya kupotea kwa USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU.
Sasa Bwana Yesu akaja,tukasoma hapo juu,kwamba imeandikwa;
" Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. " Luka 19:10

Haleluya...
Nasema,haleluya,haleluya....
Jina la Bwana Yesu lipewe sifa...

Siku ya leo nataka tujifunze jambo moja kubwa mahali hapa.
Kwamba Yesu Kristo yu hai,halisi yupo hata sasa akikuita urejee kwake,maana yupo tayari kukupokea muda wowote. Pale unapodhani ya kwamba haufai kwa sababu ya wingi wa dhambi,hapo ndipo Yeye anakuona unafaa,akikuhitaji.

Yeye mwenyewe anasema;
" ....mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. " Yoh.10:10b

Ahaaa!Kumbe...
Upo uzima ndani yake,tena si uzima tu wa kawaida bali uzima tele,uzima wa milele.
Kumbuka,
Uzima haupatikaniki katika misingi ya dini,
Uzima haupatikaniki katika kusoma sana,
Uzima haupatikaniki kwa madawa,
Wala UZIMA haupatikaniki kwa mwingine yeyote.
Bali UZIMA u ndani yake Yesu Kristo,kwa wale waliompokea kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao.

Wakati mwingine huwa sisi walokole tunalia sana,tena hasa mimi huwa ninalia si nalia kwamba mtu kaniudhi,wala!..
bali nalia pindi nikiyatafakari matendo makuu ya Mungu ndani ya maisha yangu,nasema hakika Bwana ulinipenda kwanza.
Tena huwa tunalia tunapoona watu wakipotea katika dhambi,wakati saa ya WOKOVU ndio sasa,kwamba haitajiki tena kuishi katika dhambi.

Watu hupitia katika misoto/hali ngumu sana sababu wapo nje ya system ya maisha ambayo Mungu ametukusudia kuishi.
Wengine hufikiria kwamba wamebarikiwa nje ya kanuni ya Mungu,yaani wanapoona kuwa wana mali nyingi huzani ni moja ya mbaraka wa ki-Mungu. La hasha!
Mbaraka wa ki-Mungu,ni pale roho ya mtu inapokuwa hai. roho inakuwa hai kwa kuishi maisha ya wokovu. Yeye mwenye uzima wa roho yake ndiye aliyebarikiwa...

ITAENDELEA...
* Kwa huduma ya maombi na maombezi,usisite kunipigia namba yangu hii;
0655-111149

*USIKOSE fundisho hili,maana najua kabisa lipo kusudi la msingi kwako.
UBARIKIWE.

Comments