![]() |
Dada Hawa Lufingo |
Mimi
namshukuru sana Mungu kwa kuniponya, kabla sijapata mtoto wangu wa
kwanza nilikuwa na tabia ya kula udongo pia natafuna sana mchele, hata
nilipopata mtoto bado niliendelea kula udongo na mchele, ilifikia hatua
sitamani chakula wala hamu ya kula sina nikawa nakula udongo na soda,
mchele na chai, hali ilikuja kuwa mbaya sana nilipopata mtoto wa pili
nilikuwa naweka chini ya mto mchele na udongo wakati wa kulala usiku
naamka kula, ila kuna siku kulikuwa na semina na apostle alifundisha
uzao wa nyoka, na mapepo yanavyo watumikisha watu kula
mkaa,udongo,mchele, unga wa ugali, na wakati hata nikipaka mafuta napo
hayakolei, nilivyoombewa ndo hali ilizidi kuwa mbaya, lakini nilikazana
na maombi peke yangu, siku ambayo siijui wala siikumbi nikagundua sijala
mchele wala udongo mda mrefu, Yesu alinitoa kwenye kifungo cha shetani,
saizi nipo huru, sili tena udongo wala sitafuni tena mchele, namshukulu
Mungu kwa neema alinitoa kifungoni, sasa nimenenepa na ngozi yangu ni
nzuri, Yesu amenipa mwili mpya, asante Yesu.

Comments