1.
Mathayo
18:19,20
“Tena
nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote
watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa
walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati
yao”
Nampenda
Bwana Yesu. Yani kila tukutanikapo wanadamu wawili huwa si wawili tena bali
tupo watatu. Maana Bwana Yesu hujihudhurisha kuja kuchukua maombi yetu ampe
Baba.
2.
Marko 11:22-24
“Yesu
akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote
atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni
mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu
hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo
yatakuwa yenu”
3.
Yoh. 14:13,14 ‘Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya,
ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina
langu, nitalifanya’
Msisitizo:
– Bwana Yesu anasema lolote tutakaloomba!
4.
Yoh. 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu,
ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. ”
Kukaa ndani ya Kristo na maneno yake kukaa ndani
yetu huo ni ushirika katika mahusiano yetu na Mungu. Ni ushirika wa kudumu.
Ushirika wa kila siku. Ni ushirika ambao ulianzishwa pale msalabani na Kristo
mwenyewe. Damu yake ilipomwagika pale msalabani kwa ajili ya kutusafisha dhambi
zetu, ilianzisha mahusiano yasiyo na kikomo. Kumuamini Bwana Yesu na kumkiri
kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu ni mwanzo wa mahusiano hayo ya kudumu
katika Kristo. Kuokoka ni hatua ya mwanzo. Na tunapaswa kuendelea na mahusiano
na Kristo kwa Roho Mtakatifu.
5.
Yoh. 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua
ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili
kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”
6.
Yoh 16:23,24 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin,
nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. - Hata
sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe
timilifu. -”
Hakuna masharti ya NINI TUOMBE ila
kuna masharti ya NAMNA YA KUOMBA:
i.
Kupitia jina la
Yesu
ii.
Mtu aombaye awe
na mahusiano na Mungu
iii.
Mwombaji awe na
Imani
Ubarikiwe
sana.
Comments