ASALI NDANI YA MZOGA

 Na AP Hosea Shaban: UFUFUO NA UZIMA Moshi kilimanjaro.


Wamuzi 14:1-9.
 "Samsoni akiwa na wazazi wake walitelemkia Timna, na walipofika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. Ndipo Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye samson akampasua mwanasimba kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya. Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana.

Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali. Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba."

Ni jambo gumu kusikia nyuki wanatengeneza asali ndani ya mzoga na ndivyo ilivyo katika maisha ya watu. Wapo waliotengwa na kudharauliwa, wanaonekana hawana maana lakini Mungu akiwainua kila mtu anawaheshimu. Maisha ya watu wengi mbele ya wanadamu yanaonekana kama kituko na wasio na mwelekeo, wasiostahili heshima LAKINI Mungu ndiye atawalaye ainuwaye na awezaye kubadili historia ya mtu, hata wakawa wa maana na kutamanika mbele ya watu kwani ndiye amwinuwaye amtakaye na hivyo kuwa chini kwa mtu leo haina maana atabakia hapo saa na dakika yeyote Bwana aweza kubadilisha maisha yake.

Ni maombi yangu leo kuona Mungu anakuinua na kukuketisha na wakuu, walikuona hufai waanze kukutafuta kwa sababu ya umaalum anaokuvika nao Mungu, waliokudharau wakuone wa maana kwao, waliokubeza waone aibu, watu wakuone ukiwa wa msaada kwao na maisha yako yabadilike toka kuwa chini na kwenda hali njema ya juu, Kibali cha Bwana kiwe juu yako AMENI.


AP Hosea akisoma neno



Comments