CHANZO CHA UZIMA. *Sehemu ya mwisho*

 Na Kabalama Masatu

*Kumbukumbu la Torati30:19-20* imeandikwa:-
"Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo,kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti,baraka na laana;basi chagua uzima,ili uwe hai,wewe na uzao wako;kumpenda BWANA,Mungu wako,kuitii sauti yake,na kushikamana naye;kwani hiyo ndiyo uzima wako,na wingi wa siku zako;upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako,Ibrahimu,na Isaka,na Yakobo,kuwa atawapa".

 
Mimi hili jambo nalipenda sana,hapa ninaona ni jinsi gani Mungu asivyoweza kusema uongo.Kama hapa anawakumbusha Waisrael juu ya ahadi ile aliyowaapia baba zao(Ibrahimu,Isaka na Yakobo) ya kuwapa nchi waishi kwa amani kama tu watafuata maagizo yake.


Kumbe basi mpaka leo Mungu hajasahau ahadi yake kwako wewe ambaye umekubali kuitii sauti yake (Ahadi ya uzima).
Ki ukweli ni kwamba anachotarajia akione Mungu kwa mwanadamu wa leo ni maamuzi sahihi ya kumjua yeye ili apate uzima.


Katika #Yohana17:3 imeandikwa:-
"Na uzima wa milele ndio huu,wakujue wewe,Mungu wa pekee wa kweli,na Yesu Kristo uliyemtuma".
Hili ni jambo la kuangalia sana.
Kama andiko linaniambia ya kwamba "uzima wa milele ni kumjua Mungu wa kweli";basi vile vile tutambue ya kwamba ukimjua Mungu wa uongo basi mauti inakuhusu.
Bado nashauri kuchunguza uamuzi wetu ili tusije tukaishia kwenye mauti.


Utambue ya kwamba chanzo cha uzima siyo kuwa maarufu,siyo kuwajua waganga wengi,siyo kuwa maarufu kwa uzinzi bali ni kuitiisha nafsi yako imjue Bwana,Mungu wako aliye wa kweli yeye aliyemtuma Yesu Kristo ili wote tuokolewe kutoka kwenye dhambi.
#NB: Hakuna kingine chenye kukuokoa wewe na mauti(laana) isipokuwa kumjua Mungu wa kweli nawe ukakubali kuitiisha nafsi yako kwa kushikamana na mwokozi wako ambaye atakuokoa na mauti isikupate.


                         MUNGU akubariki sana.

                             By Kabalama Masatu                                

                                  Mawasiliano ni:-
                                      0753-305957;
                                       0789-628226;
                                          0717-624035
 

                                           ***MWISHO****.

Comments