Jitahidi kuhakikisha unalinda moyo
wako na moyo wa mpenzi wako; usije ukaupasua na kuuumiza.

Kutoshughulikia vizuri tatizo lolote
kwenye ndoa hupelekea Chuki, Uchungu, Kinyongo, Kuumia hisia na huweza
kusababisha mwanandoa mmoja kujiondoa katika muungano wa kindoa uliopo (kuanza
kuishi kivyake katika kufikiria na kutenda).
Zifuatazo ni dalili
mbaya sana ambazo zinaonesha ndoa inayoelekea kwenye kifo
KUFIKIRIA MAISHA
KIVYAKO BILA MKE AU MUME KUMUHUSISHA
Ukiona unaanza kufikiria uzuri wa
maisha utakavyokuwa bila mwenzi wako kwa maana kwamba kuwa na yeye unaona
asilimia mia moja anakulostisha, au hana maana kabisa ni dalili kwamba hiyo
ndoa inaelekea kwenye kifo cha ghafla. Na kama unasongwa sana na mawazo kutaka
kuishi mwenye au na mtu mwingine zaidi ya huyo uliye naye na kujiona utakuwa na
amani zaidi basi unaelekea kubaya kwani inaonesha umeshapoteza nafasi yake
ndani ya moyo wako na kitu cha msingi waone washauri wa mambo ya ndoa ili
waweze kukusaidia.
MAMBO
MABAYA NI MENGI KULIKO MAMBO MAZURI KWENYE NDOA YAKO
Kama mnajikuta ndoa yenu ina mambo
mabaya mengi zaidi kama vile kutokuelewana, kila mtu ana hasira, mnapishana
lugha kila mara, hakuna kucheka wala kufurahishana na mambo mazuri kama kucheka
pamoja, kufurahi pamoja, kujisikia bila mwenzako siku haiendi basi hiyo ni
dalili kwamba hiyo ndoa inahitaji msaada na bila kuifanyia ukarabati basi
itasombwa na mafuriko na hatimaye kufa.
UNAJISIKIA VIGUMU
SANA KUWASILIANA NA MKE AU MUME WAKO
Je, unajisikia kupatwa na hofu au
mashaka kuongea na mke au mume wako kuhusu matatizo ya ndoa yako au maisha yenu
kwa ujumla? Mawasiliano ndiyo njia pekee ya kuondoa stress za ndoa na maisha
kwa ujumla na hatimaye kujenga ndoa yenye afya kwa wanandoa. Kama mkiwa pamoja
mnakuwa kimya bila kuongea chochote na hakuna dalili ya kutaka kuongea na
mwenzako basi kuna tatizo kubwa sana, hasa kama ni tofauti sana na kawaida yenu
hasa jinsi ilivyokuwa katika siku za kwanza wakati mnachumbiana. Kama hujisikii
vizuri kuwasiliana na mwanandoa mwenzio basi hiyo ni dalili kwamba tayari
umekosa imani kwake na ndoa huwa inakuwa katika wakati mgumu kukiwa kauna
kuaminiana (trust) Pia kama wewe ni mtu wa mwisho kujua kitu chochote muhimu au
kuzuri kuhusu yeye, basi hapo kuna tatizo kwani ni kawaida wanandoa kuelezana
vitu vizuri vinavyotokea kwa mmoja wao.
KILA
MMOJA KUKATAA KUHUSIKA NA MATATIZO AU MIGOGORO YA NDOA INAPOJITOKEZA
Kama kila mmoja anajilinda na
kutothamini hisia za mwenzake hasa linapotokea tatizo na kuanza kumrushia
mwenzake lawana kwamba ndiye muhusika na wote mnakuwa na msimamo huohuo, fahamu
kwamba hapo ndoa inapitiliza hata tiba za uangalifu zinazopatikana ICU. Ikiwa
migogoro au matatizo yanapojitokeza kuna kuwa na kushindana kwa kila mmoja
kukwepa kuhusika na badala ya kupata suluhisho mnajikuta mgogoro unazidi
kuongezeka basi hiyo ni dalili kwamba sasa mmeanza kubusu kifo cha ndoa.
KUJIKUTA
NI WEWE PEKE YAKO TU UNAHUSIKA KATIKA KUTATUA MIGOGORO AU MATATIZO YA NDOA.
Je, umekata tamaa, au kujisikia
vibaya kuongea masuala ya matatizo ya ndoa yako kwa sababu mwenzako
anakurudisha nyumba, au imefika mahali na wewe umeamua kunyamaza na kuachana
kabisa na kujishughulisha na tatizo lolote katika ndoa na matokeo yake hakuna
hata mmoja anajali tena kushungulikia matatizo ya ndoa? Kama mpo kwenye
matatizo na kila mmoja amenyamaza kimya katika kuhakikisha mnamaliza tatizo
lililopo basi hii ndoa ipo ICU na kama mtabaki kimya bila kila mmoja wenu
kuhusika ili kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari basi ni kama bomu lililotegwa
ardhini na siku mtu akikanyaga hakuna kitakachosalia.
TENDO LA NDOA
Kama mmoja wenu sasa hana hamu
kabisa na tendo la ndoa, au wote kwa pamoja hamna hamu kabisa ya tendo la ndoa
hiyo ni dalili kwamba somethings is wrong. Kukosa faragha ya pamoja (intimacy
and affection) itawafikisha mahali ambapo ndoa inaweza kufa au kuwa na ndoa
isiyokidhi haja au kukosa kuridhishana inavyotakiwa.
MAOMBI NI MUHIMU SANA KWA WANANDOA.
Comments