BWANA YESU
asifiwe ndugu yangu.
Karibu
tujifunze ujumbe huu kuhusu kuzini,
jambo ambalo huwakosesha wengi sana.
-Kuzini ni
kitendo cha kufanya mapenzi ambacho ni dhambi.
-Anayezini
ni kahaba, mwasherati , Malaya, changudoa na mzinzi.
-Mzinzi ni
mtu aliyeoa au kuolewa anapozini na mtu ambaye siye mkewe au mmewe.
-Mwasherati
ni mtu Yule asiyeoa au kuolewa anapozini na mtu na mtu mwingine huo ndio
uasherati.
-Kahaba ni
mtu Yule anayezini na watu wengi au kujiuza kwa lengo la kujipatia kipato.
1 Kor 6:18 (Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake;
ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
).
-Watu wengi
kwa sababu ya uzinzi wao au uasherati wao huitwa viwembe.
Hii ni
dhambi mbaya ana Kumb 5:18 MUNGU anasema ‘’ Wala Usizini’’
-Dhambi hii
imewaharibia wengi uhusianao wao na MUNGU.
-Wengi
wamekosa Baraka zao kwa sababu ya uzinzi.
-Wengi
wamekufa kwa sababu ya kuzini.
-Wengi wako
kuzimu sababu ya kuzini.
-Kuzini ni
jambo baya sana.
VYANZO VYA UZINZI.
1.
Chanzo
cha kwanza cha uzinzi ni TAMAA.
Kumb 5:21 ( Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani
yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala
ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani
yako.
).
Usitamani mke wa jirani yako, tamaa hii ya wake za watu ni mbaya sana ni ni chanzo kikubwa cha uzinzi.
Yakobo 1:13-15 ( Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na MUNGU; maana MUNGU hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
).
Tamaa ikiwa ndani yao inauwezo wa kunena na kuongea , pia shetani anaanza
kukuhubiri juu ya kufanya uovu.
Tamaa inazaa dhambi, dhambi inazaa mauti.
Tamaa ndi mbaya sana.
Mathayo 5:27-32( Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Jicho lako la kuume
likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo
chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Na mkono wako wa kuume
ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako
kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
lakini mimi nawaambia, Kila
mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa
mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
)
2. Chanzo cha tatu cha uzinzi ni MAVAZI
1 Petro 3:1-5 ( Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako
wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
bali kuwe utu wa moyoni
usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na
utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za MUNGU.
Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini MUNGU, na kuwatii waume zao.
).
mavazi ya kujistiri ni muhimu sana.
Yeremia 31:22 (Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.
).
Mwanamke anatakiwa amlinde mwanaume kwa kutovaa nguo za mitego.
3. Chanzo cha 3 cha uzinzi ni KUKAA
SEHEMU MOJA KWA MUDA MREFU MKIWA WAWILI TU WA JINSIA TOFAUTI.
Wagalatia 5:16 (Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
).
Mithali 15:1-2 ( Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.).
4. Chanzo cha pili cha
uzinzi ni UBINAFSI.
Ubinafsi humfanya mtu awe anataka kila msichana/ mvulana awe wake.
Ubinafsi humfanya mtu kujipendelea kila kitu na hivyo huwafanya wabinafsi
wengi kujipendelea pia kutenda dhambi hii.
Unamuona msichana amejitunza na wewe moyoni mwako unawaza kwamba
anatayemuona msichana huyu atafaidi sana na hiyo inakupelekea kutaka kumwoa
kwanza wewe huyo msichana kabla hajaolewa na mtu sahihi. Na kama msichana huyo
naye hana hofu ya MUNGU ndio kabisa wewe pamoja na ubinafsi wako mnazaa dhambi
na dhambi hiyo inakuwa na madhara kwako na kumharibia maisha msichana wa watu.
5.Chanzo cha 5 cha uzinzi ni KUWA KATIKA ENEO AMBALO HUTAKIWI KUWA KWA
WAKATI HUO.
2 Samweli 11:1-12 (Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani,
Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote;
wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. Lakini Daudi mwenyewe
akakaa Yerusalemu.
Ikawa wakati wa jioni, Daudi
akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na
alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa
mzuri sana, wa kupendeza macho.
Naye Daudi akapeleka, akauliza
habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba,
binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
Basi Daudi akapeleka wajumbe,
akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke
amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.
Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito.
Ndipo Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, Unipelekee Uria, Mhiti. Naye Yoabu akampeleka Uria kwa Daudi.
Uria alipomwendea Daudi, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, na habari za watu, na habari za vita.
Daudi akamwambia Uria, Haya,
shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako. Basi Uria akatoka katika
nyumba ya mfalme, na tunu ya vyakula ikamfuata, iliyotoka kwa mfalme.
Lakini Uria akalala mlangoni pa nyumba ya mfalme, pamoja na watumishi wote wa bwana wake, wala hakushuka nyumbani kwake.
Watu walipomwambia Daudi ya
kwamba, Uria hakushuka nyumbani kwake, Daudi akamwambia Uria, Je!
Hukutoka safarini? Mbona hukushuka nyumbani kwako?
Naye Uria akamwambia Daudi,
Sanduku, na Israeli, na Yuda, wanakaa vibandani; na bwana wangu Yoabu,
na watumishi wa bwana wangu, wamepiga kambi waziwazi uwandani; nami
niende nyumbani kwangu, kula na kunywa, na kulala na mke wangu?
Uishivyo, na kama roho yako iishivyo, mimi sitafanya jambo hili.
Basi Daudi akamwambia Uria,
Ngoja hapa leo tena, na kesho nitakuacha kwenda zako. Basi Uria akakaa
Yerusalemu siku ile, na siku ya pili yake.
)
Daudi alikaa katika eneo ambalo sio sahihi na ikapelekea uzinzi, hata leo wapo watu hukaa kwenye mitego ya watu wabaya na kupelekea uzinzi.
Waefeso 5:15-17 (Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
).
6. Chanzo cha 6 cha Uzinzi ni MAZUNGUMZO YASIYO NA KIASI.
Mazungumzo yasiyo na kiasi ni mabaya sana maana adui kidogo kidogo
ataanza kuwawekea dhambi ndani ya mioyo yenu. Ndio maana unatakiwa kuwa na
kiasi maana shetani yuko vitani ili akuangamize. Wengi wameongea hadi story
nzuri zikaisha na kuanza kuongea pumba tu na kuwapelekea dhambi.
7. Chanzo cha 7 cha uzinzi ni KUIGA
Wadada wengi wamepata mimba na kuharibiwa mosomo
yao kwa kuiga kutoka kwa wenzao ambao
shetani amewavaa na kufanya uovu huu.
Sio kila
jambo ni la kuiga mengine ni mambo mabaya na ya kifo.
MUNGU anautazamaje uzinzi.
1.Uzinzi ni ubaya mkubwa.
2.
Uzinzi
ni jeraha la fedheha.
(Mithali
6: 32-33 ( Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
)
EPUKA DHAMBI YA UZINZI.
1 Kor 6:9-10
( Au hamjui ya kuwa wadhalimu
hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi
ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala
walawiti,
wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
).
Ufunuo 21 :8
(Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na
wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika
lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
).
Mithali 1:28
-31 (Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA.
Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote.
Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe.
).
Comments