EPHRAIM SEKELETI KUMBEBA ROSE MUHANDO.- AGOSTI 3


Muimbaji mahiri wa muziki wa Injili, Ephraim Sekeleti, atatumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Kamata Pindo la Yesu ya Rose Muhando Agosti 3, mwaka huu.



Taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Rose Muhando jana, ilieleza kuwa tayari Kampuni
ya Msama Promotions inayodhamini uzinduzi wake imeshamalizana na mwimbaji huyo.



“Nashukuru sana Msama Promotions kwa udhamini wao, na jana (juzi) wamenihakikishia wameshamalizana na Sekeleti na amekubali kuja kuungana nami katika uzinduzi wangu.



“Ni msanii mwenye uwezo mkubwa, ambaye mashabiki wangu watapenda kuja kumuona jukwaani,” alisema mwimbaji huyo na kuzitaja baadhi ya nyimbo maarufu za Sekeleti kuwa ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu.



Uzinduzi wa albamu hiyo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Agosti 3, mwaka huu na kisha Agosti 10 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Waimbaji wengine ambao hadi sasa wameshathibitisha kushiriki uzinduzi huo ni Upendo Nkone, John Lissu na Bonny Mwaitege, huku wasanii wengine mahiri wakitarajiwa nao kuthibitisha ushiriki wao siku za usoni.

Comments