FAHAMU JINSI MUNGU ALIVYOJIFUNUA ZAMANI, NA JINSI ALIVYOJIFUNUA KATIKA NYAKATI HIZI TULIZONAZO

Bwana Yesu asifiwe wapendwa!. 

Mungu wetu ni Mungu ambaye amejifunua kwetu kwa nyakati mbili tofauti, 
wakati wa agano la kale na wakati wa agano jipya. 

Na Mtumishi Alex
Lakini pamoja na kujifunua kwa nyakati mbili na kwa njia tofauti bado Mungu wetu hajabadilika, ni yule yule jana, leo, na hata milele. 

Katika AGANO LA KALE, MUNGU alisema na watu wake kwa njia ya manabii katika sehemu kubwa, lakin katika AGANO JIPYA, MUNGU anasema na watu wake kupitia KRISTO YESU, hii ndiyo njia pekee ambayo Mungu amejifunua katika nyakati hizi tulizonazo. Hebu tuangalie biblia inasemaje "WAIBRANIA 1:1-2 Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi anasema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote tena kwa yeye aliufanya ulimwengu".  

Ndungu mpendwa katika KRISTO YESU, tamani sana kusema na Bwana YESU katika maisha yako kuliko kitu kingine chochote. 

Barikiwa sana.
 By ALEX wa YESU.

Comments