HAIBA ZA WANANDOA!

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Wanandoa wakifanana Haiba zao nini Hutokea katika Mahusiano yao?

1. Sangwine na Sangwine wakioana = moto lazima uwake – ila huwa hawaachani haraka. Wanagombana sana na kufukuzana sana lakini mwishowe wanarudiana.
Wanauwezo mkubwa sana katika mambo ya tendo la ndoa hulifanya kwa kufurahia kwa kiwango cha juu kuliko makundi mengine.


2. Koreliki na Koreliki wakioana ndoa zao maranyingi huwa hazidumu kwa muda mrefu, na huishia kuachana kwa ugomvi na maumivu makali sana.
Wanaongoza kwa kutojua kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi. Mara nyingi hubakia na njaa ya muda mrefu ambayo baadaye husababisha matatizo mengine katika mahusiano yao. Sio wazuri katika mambo ya mahusiano ya kimapenzi.


3. Mwanamke katika haiba ya Koreliki, anapoachana na mumewe, mara nyingi huwa hatamani na hataki kabisa kuolewa au kuishi na mwanaume mwingine tena. Huamua kujitengenezea maisha yake yeye kama yeye na kulea watoto wake bila kutamani kuwa chini ya mamlaka ya mume.

4. Melankoli na Melanloli wakioana wanaweza wasiachane, lakini huwa wanaishi maisha kama ya maigizo. Wanaweza kuishi nyummba moja lakini hawalali chumba kimoja au kitanda kimoja. Kama itatokea wamelala kitanda kimoja basi ujue kila mtu na hamsini zake. Pia katika maisha ya mahusiano ya tendo la ndoa huwa sio wazuri sana. Ila mmoja wapo anapoamua kuhusika katika tendo hilo hulifanya kwa kudhamilia na huwa zuri sana lakini mara nyingi hawana dhamira kama hiyo kulinganisha na haiba kama ya Sangwini.

5. Ugomvi wao hauwezi kamwe kuusikia nje, hata ndugu wa karibu wakati mwingine wanaweza wasijue kama kuna tatizo katika ndoa hiyo.

6. Wanandoa wenye haiba hii, Mara nyingi huweka mazingira ya usiri wa hali ya juu sana. 

7. Ndoa ya Melankoli na Melankoli, mara nyingi huwa na maumivu makali sana ya ndani ya moyo, na hujitahidi kujionyesha kwa nje kama ni watu wenye mafanikio sana na wasio na matatizo yeyote katika mahusiano yao. Kwa kawaida hufunika donda sugu na kitambaa cha nguo safi.

8. Fregmatiki na Fregmatiki wakiona ni mara chache sana kukuta wanatimiza malengo yao katika maisha. Mara nyingi huwa hawafikii malengo yao kutokana na haiba yao ya upole na ukimya na kutotaka kukosana na watu. Wanafanya vizuri sana katika mambo ya tendo la Ndoa wakifuatia baada ya kundi la Sangwini.

9. Maisha ya wanandoa wenye haiba ya Fregmatik hujawa na huruma na kutaka kumpendeza kila mtu atakaye kuwa mbele yake.

10. Ingawa maisha ya wanandoa ya haiba ya Fregmatiki huwa na wakati mgumu sana kimaendeleo, maisha yao kimahusiano huwa mazuri sana kama mume na mke. Ni watu wenye msimamo wasio weza kutekwa kwa urahisi.

NI HAIBA GANI IKIOANA NA HAIBA FULANI NDIO NDOA ITAKUWA NA AMANI
JIPATIE KITABU CHAKU KUJUA ZAIDI

Comments