HIGHER LEVELS CONFERENCE KATIKA MATUKIO


 Mtume Onesmo Ndegi, mwenyeji wa Kongamano hilo
Zilikuwa ni siku sita za kwenda viwango vya juu katika Jiji la Dar es salam Katika Kanisa la Living Waters Centre chini ya mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi, kwenye 'Kongamano la Viwango vya Juu' (Higher Levels Conference)

Kila mwaka kwenye Kanisa la Living Waters Centre huwa kuna Kongamano kuu ambalo linakuwa na watumishi wa Mungu kutoka makanisa mbalimbali nchini na nje ya nchi, ambapo kwa mwaka huu alikuwepo Askofu Kameta wa Dar es salaam, Askofu Oram Mustafa kutoka Arusha, Mchungaji Titus Mkama wa Ilala TAG Dar es Salaam, Askofu Dkt Peter Muteba wa Afrika Kusini, Askofu Dkt Tengu Yoka kutoka Nairobi, Mtume Aaron Timoth wa DRC, na wenyeji Mtume Onesmo na Mwalimu Lilian Ndegi, ambapo watu walipata muda wa kutosha kujifunza Neno la Mungu kwa ufasaha na kuombewa na watumishi wote waliohudumu katika Kongamano hilo.

Living Waters Praise Team, Totoo, Kwaya kutoka Glory Land Arusha, na kwaya kutoka Nairobi walipata kuhudumu kwenye kongamano hilo, huku pia King Chavala akiwepo kufanya vitu vyake.
Askofu Oram Mustafa kutoka Arusha, Gloryland International Church
Mchungaji Titus Mkama wa Ilala TAG Dar es Salaam
Askofu Dkt. Peter Muteba, Afrika Kusini

Askofu Dkt. Tengu Yoka kutoka Nairobi

Living Waters Praise Team walipokuwa wakihudumu katika Kongamano hilo
Askofu Dkt Peter Muteba na mkewe

Comments