HUKUMU KWA WENYE MIZAHA.

Na Lucy Marandu.

Mithali 19:29

Imekuwa ni kawaida sana kwetu kuona watu walio OKOKA KUFANYA MIZAHA, MCHANA KWEUPE!

Mtunga zaburi(Daudi) alizungumza mapema akasema; Heri mtu yule asiyeenda katika Shauri la wasiyo haki wala KUKETI BARAZANI PA WENYE MIZAHA..
Zab 1:1-2


IPO MIZAHA KATIKA MANENO:
Mfalme Suleiman akasema; Azuiyaye maneno yake ni mwenye akili na maarifa
Mithali 10:19, 17:27a


YESU akasema; Kila neno lisilo maana watakalolinena wanadamu watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu....
Mt 12:36-37. Nk


LAKINI PIA, IPO MIZAHA KATIKA MATENDO YETU

Paulo mtume akasema; Lakini uasherati usitatwe kwetu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote wa kutamani, kama IWASTAHILIVYO WATAKATIFU
Efe 5:3-4


Tunaona mizaha katika mavazi yetu tuyavaayo(hususani sisi akina dada) ambayo huchochea hisia za mapenzi kwa watu ya jinsia tofauti nasi, kiasi kwamba imekuwa ni ngumu sana kutofautisha ni nani kahaba na ni nani mwana wa Mungu!

Utakuta mlokole anapita kivyake kwenye vijiwe vya wahuni! Au mitaani tuu! Unasikia milio psiii psiii psiiii oya wewe shost, sema mrembo nk! Kimsingi miito hii huwa inategemeana sana na jinsi ulivyo na mwonekano wako au mtazamo wako kwa ujumla wake nk!

Sidhani ikiwa umevaa kiheshima kabisa ukasindikizwa na milio hii! Ijapokuwa pia wapo wanaume wasio wastaarabu hata kama umevaa kwa heshima bado watakuita kwa milio hiyo hiyo japo siyo saaana kama ambavyo ungevaa kihuni!

Rafiki yangu mpendwa ni bora ukawa umevaa kwa heshima, halafu milio hiyo ikapigwa juu yako, kwani hapo yule apigaye miluzi ndiye atakayeonekana chizi au mwenye Mizaha, lakini ukiwa wewe umevalia isivyo, kwa vyovyote vile kila mtu akuonaye anaona umejitakia kwa kukaribisha Mizaha ndani yk!

Hivyo tuwe makini sana wana wa Mungu, kujitofautisha na Makahaba! Biblia inasema imetupasa KUMPENDEZA MUNGU PAMOJA NA WANADAMU SIKU ZOTE!
Mdo 24:16
2kor 8:20


Ubarikiwe kipekee wewe uliyeusoma ujumbe huu na kudhamiria kubadilika kuanzia leo katika Jiiiiiina la Yesu! 

Ameen.
MUNGU akubariki sana.
By Lucy Marandu.

Comments