IMETUPASA KUTANGATANGA ILI KUTAFUTA MALISHO BORA YA ROHO ZETU.


Zab 59:15, Zab 107:4-5, 7, 9

Wapendwa, kwa nini tuzidiwe akili na wanyama? Ili hali Mungu wetu alituumba wathamani na wenye akili/mamlaka kuliko viumbe wotee?? Mwa 1:28

Ni kichekesho sn, Wanyama mfano ng'ombe wanajua kusoma alama za nyakati kuliko Mwanadam!

Ng'ombe akiona hapa hamna malisho ya kutosha anahama na kwenda kutafuta malisho sehemu nyingine! Lakini binadamu wa sasa wananichekesha sana tena sana, eti utakuta yuko hoi taaabani (kiroho) yaani anaenda kudondoka kutokana na utapiamlo wa kiroho alo nao lakini utamsikia; OOOOOH MIMI SIWEZI KABISA KUTANGA TANGA, NA KUIACHA DINI YA WAZAZI WANGU! Ha ha ha haaa...

Rafiki yangu mpendwa, acha kujidanganya na kujitaabisha na mambo yasiyo na msingi! Hivi nikuulize ni wapi palipoandikwa SHIKA SANA DINI YAKOO?? Bila shaka hakuna popote palipoandikwa hivyo, Soma kuanzia mwanzo hadi ufunuo! Biblia inasema shika sana ulichonacho.... ambacho ni NENO LA MUNGU
Ufu 3:10-12

Kumbuka, Suala la kutanga tanga halikuanza kwangu au kwako, hata Mtume Paulo aliiacha dini yake nzuri na kumfuata Yesu Gal 1:14-16!

INACHEKESHA SANA, Mtu ana uwezo wa kumhamisha mtoto wake shule, hata mara mbili, au mara tatu kwa madai anamtafutia elimu bora zaidi! Lakini mtu huyo huyo anashindwa kujitafutia malisho bora kwa ajili ya kiroho chake ambacho ni cha thamani sn maishani mwake, maana ni kitu kitakachogharimu maisha yake yote baada ya maisha haya ya sasa! Ebr 9:27

Rafiki yangu mpendwa, nikupendaye! Ninakusihi sana tena sana, kuanzia sasa, Anza kutamani kumjua Kristo kwa undani wake, Tafuta kanisa linalohubiri WOKOVU kisha ingia pale na ujifunze nini maana ya kuokoka, Jee kweli kuna kuokoka dunianii?? Jee kuna tofauti gani katika ya dini na Kumpokea Yesu nk... Utapata kujua mengi na bila shaka utafanya uamuzi wa Busara!

Biblia Inasema; KHERI WENYE NJAA NA KIU YA HAKI, MAANA HAO WATASHIBISHWA, Matayo 5:6
*Na kwa kuwa umeonyesha nia ya kutamani kujua, Hakika Mungu sii mwongo atakushibisha bila shaka! Ameen

Mungu wa Mbinguni na akubariki sn, wewe ambaye utayafanyia kazi maneno haya!

Shaloom Shaloom!

By Lucy Marandu.

Comments