JE !!! UMEJIANDAAJE KUKUTANA NA MUNGU ???


Watu wengi wanapenda kumwona Mungu, lakini wanashindwa kumwona Mungu kwa kutofahamu vizuizi viwafanyao wasimwone Mungu maishani mwao. Je, umewahi kujiuliza “kwanini watu wengi hukata tamaa na kuhisi kama Mungu hayupo, au Mungu amewaacha?” ebu tuangalie kwa Pamoja,
Maandiko matakatifu yanasema “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana yamambo yasiyoonekana,” (Waebrania 11:1). “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza,
Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao,” (Waebrania 11:6)

Mungu ametukaribia sana kwa kumtuma mwanae Yesu kuutoa uhai wake kwa ajili Yetu sote na siku zote anazidi kukaribia watu wote.
Maana yeye ni Yehova, Mungu wetu, na hushika mkono wetu wa kuume na kutuambia, usiogope, nitakusaidia. lakini wanadamu wanaangamia,wanapotea na wachache sana wanaoingia ufalme wa Mungu.”kama ilivyoandikwa (Mat.7:14:Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyo ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.’’)
Tunaweza kusema kuamini ni KUJISALIMISHA KWA MUNGU . Mtu unapojisalimisha, huwa hakuna unachobakiza. Unajitoa kabisa kwa yule unayejisalimisha kwake ili akutendee apendavyo. Ni hakika tunahitaji kujisalimisha kwa Mungu ili atutendee kama apendavyo. Na tunafanya hivyo kwa kujua wazi kile anachotaka kutufanyia kwa kuwa yeye ni mwaminifu, tofauti na ambavyo unaweza kufanya kwa mwanadamu anayebadilika-badilika. Imani kwa Mungu ni jambo la hakika (soma Waebrania11:1).
Lakini Jeshi la mapepo wanakimbia kimbia huko na huku kwasababu wanajua muda wao karibu kwisha, kwasababu muda wa kuwaharibu/kuwapoteza wanadamu unakaribia kufungwa. Wamebeba silaha za kuharibu watu na kuwapeleka kuzimu.
Hivyo imetupasa kupokea imani yote kama tulivyohubiriwa na kufundishwa na KWA KADRI YA ROHO MTAKATIFU maana Neno lasema Yoh12:48.Yuko amhukumuye yeye anikataaye Mimi na kutokuyapokea maneno Yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.

Hivyo kuzimu ni halisi na Mbingu ipo. “lakini kuzimu haikuwekwa na Mungu kwaajiliya wanadamu bali kwajili ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini,kwasababu ya dhambi na kukosekana kwa toba, wanadamu wataishia huko kuzimu, na ni wengiwataangamia kuliko watakaofika katika utukufu wa MUNGU yamkini wengine ni ndugu wa damu, Yesu kristo alitoa maisha kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie [Kuzimu]bali ni kwa upendo na huruma, ili wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme waMbinguni.” Yesu anaiangalia dunia kwa huzuni na huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu, kadri aonavyo watu wanaendelea kuasi.
Yapo mambo mengi yatakayowazuia wanadamu leo kuingia ufalme wa Mbinguni.lakini nitazungumzia baadhi tu.
1. Kusamehe na unyenyekevu
Kusamehe nilazima kwasababu Yeye alitusamehe makosa yetu yote, na ndiyo maana wengi tupona amani ya Kristo ndani yetu, lakini ukishindwa kusamehena na ukiwa na chuki miongoni mwa watakatifu wa Bwana, tuache malaumu, mafundisho ya mabaya, masengenyo, kwa kuwa ni muda wa kusamehe! Bila kusamehe ujue utakwenda kuzimu, kwakuwa hakuna awezaye kununua maisha. Hakuna aliyejilipia gharama mwenyewe isipokuwa YESU KRISTO pale kalvari na ameagiza kwenye maelezo ya the said sala ya Bwana pale kwenye Mathayo kwa kuwa yeye alikuwa wa kwanza kusamehe kalvary. Kuna nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawajafa, walio hai, wanaomuda wa kutubu!
Unyenyekevu ndio uliomfanya Musa amwone Mungu ktk maisha yake ebu ona hapa

KUTOKA 33:11BWANA akazungumza na Mose uso kwa uso, kama vile mtu azungumzavyo na rafiki yake. Kisha Mose akarudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka mle hemani. Na kuonyesha kwamba kakutana na Mungu alinga’aa sehemu za paji la uso wake na watu walishindwa kuvumilia uwepo wa BWANA kwa kumwangalia kwa Muda mrefu.
KUMBUKUMBU LA TORATI 34:10 na ktk Israel hajatokea mtu aliyepata kuzungumza uso kwa uso na Mungu. Na zipo sifa zile ambazo Mungu amezisema mwenyewe kwamba alifanya hivyo kwa Musa kwa sababu alikuwa mtiifu,mnyenyekevu asiye na kiburi n.k. Alitii neno akafanya kama lilivyo. Lakini siku izi Mungu akikuinua mtumishi kidogo tu unakuwa hushikiki na hata unaanza kuuza hata kipawa cha Mungu kwa pesa. Ati kwamba una pesa ngapi uombewe?
2. Bize na dunia.
Watu wengi maarufu(waigizaji wanamuziki, wachungaji, maaskofu, mapadri, mapapa, maraisi nk) wataenda kuzimu kwa sababu wanatumia mda mwingi sana kuwa duniani kwa kumsaidia ibilisi. Tunakuta wanamuziki maarufu sana duniani wakifanya miziki isiyo na tija kwa wanadamu na kuwafanya watu dunia nzima kufuata mambo yanayoimbwa humo.
Neno linasema Zaburi 11:6 Juu ya waovu atawanyeshea makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.. Ujira wa asiye tubu. Maana kazi wanazozifanya hazina ujira kwa Mungu wetu.
Hivyo kama ilivyo andikwa 1yohana2:15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Wapo watu wengi maarufu na wanaijua kweli na tena wengi ni Maaskofu wachungaji kwa makusudi wanaipotosha kweli ili waendelee kuwa na washirika wasio watakatifu na wala hawakusema kweli kama ilivyo japo kweli waliijua ila wanapenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za kweli ya wokovu. Hawatoi uhalisi wa injili bali wamepindisha wanavyotaka wao si kama Mungu atakavyo.
Tukumbuke kwamba haipo nafasi ya kurudi duniani, ili tutubu ukifa ni basi.
Wapo watu wengi wanaongoza makanisa makubwa sana kwa umati mkubwa na huku wakiabudu sanamu.
Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa bali ni YESU pekee awezaye kuokoa, na nje yake hakuna mwingine aokoaye. anawapenda wenye dhambi, lakini anachukia dhambi.
NI WAKATI WAKO KUCHUKUA HATUA SASA KUJIANDAA KUKUTANA NA MUNGU.
FIKIRI ikiwa unapata nafasi ya kukutana na MUNGU sasa hivi UTAMWAMBIA NINI ??????
MUNGU akubariki sana .
By Faith Kaingu

Comments