JIFUNZE NAMBA SABA KATIKA MAANDIKO

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Namba saba ni namba ya UKAMILIFU NA UTOSHELEVU.

Ninamuomba Mungu Akamilishe na kukupa utosherevu katika mwezi huu wa 7
Katika tafsiri ya Ki-Ebrania ina maanisha kuwa ni namba iliyo kamilika, inayojitosheleza.

Katika kitabu cha Ufunuo;
1. Kuna Makanisa SABA.
2. Kuna Matarumbeta SABA
3. Kuna vitasa SABA (Ufunuo 17:1)
4. Kuna watu SABA.
5. Kuna maangamizi SABA
6. Baada ya kukamilisha uumbaji Mungu alipumzika katika siku ya SABA
(Mwz 2:2-3)
7. Kuna maraika SABA wenye mapigo SABA (Ufunuo 5:1)
8. Neno “Yesu” linapatikana mara SABA katika Ufunuo.
9. Yusufu alitabiri juu ya miaka SABA ya mavuno na miaka saba ya njaa.
10. (Mwanzo 41:1-57)
11. Namba ya Mungu katika kusamehe ni SABA x SABA kwa siku (Mt 18:21).
12. Mungu alisema angewapiga Israel mara SABA kwaajili ya dhambi zao.
(Walawi 26:24)
13. Mungu alisema mtu yeyote atakaye muua Kaini atalipiziwa mara SABA
(Mwz 4:15)
14. Kuna mambo SABA ya thamani katika kitabu cha Petero. (Petero 1:7,19, 2:4-7).
15. Naamani aliambiwa akaoge mara saba katika mto Jordani ndipo atakasike. “Naye Elisha akampelekea ujumbe, akisema, enenda ukaoge katika Yorodani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia tena. Nawe utakuwa safi.” (2Wafalme 5:10)

16. Miujiza SABA imerekodiwa katika injili ya Yohana.
17. Neno “Wimbo Mpya” limetokea mara SABA katika Agano la Kale
18. Neno “Yesu Akasema” limetajwa mara SABA katika Injiri (Lu 23:34,43; Yoh 19:27; Mt 27:46; Yoh 19:28,30; Lu 23:46)
19. Maombolezo kwaajili ya Yakobo yalikwisha baada ya siku SABA (Mwz 50:10)
20. Pigo la maji kuwa damu kule Misri lilimalizika baada ya siku SABA (Kutoka 7:25)
21. Israel walizunguka ukuta wa Yeriko kwa muda wa siku SABA na siku ya SABA walizunguka mara SABA (Jos 6:4)
22. Pasaka katika Agano la Kale ilidumu kwa muda wa siku SABA (Kutoka 12:15)
23. Sauli alielekezwa na Samweli kukaa pale Gilgali akisubiri amri ya Nabii kwa muda wa siku SABA (1Samweli 10:8)
24. Karamu katika hema ya Musa ilidumu kwa muda wa siku SABA (Wal 23:34,42)
25. Unajisi katika Agano la Kale ulidumu kwa muda wa siku SABA (Wal 12:2; 13:4)
26. Mfalme Daudi alifunga akiomba kwaajili ya mtoto wake kwa muda wa siku SABA (2Sam 12:16,18,22)
27. Mifugo katika Agano la kale ilipaswa kubakia kwa mama zao kwa siku SABA ndipo itolewe kwa Bwana. (Kutoka 22:30)
28. Njaa katika Kanani ilidumu kwa muda wa miaka SABA (2Sam 24:13; 2Ki 8:1)
29. Maadui wakikujia kwa njia moja Bwna atawatawanya kwa njia SABA
(Kumb 28:25)
• Kuna vitu 7 vilivyo funnuliwa
i. Hands, for benevolence (Kumb 15:8)
ii. Macho kwaajili ya maono (2Wafal 6:17)
iii. Masikio kwaajili ya kusikia (Zab 40:6)
iv. Midomo kwajili ya ushuhuda (Zab 51:15)
v. Madilisha kwaajili ya maombi (Dan 6:10)
vi. Moyo kwaajili ya ujumbe wa Mungu (Mdo 16:14)
vii. Milango kwaajili ya huduma (2Cor 2:12)

30. Yakobo alitumikia miaka SABA ndipo ampate Raheri (Mwz 29:20)
31. Fedha ilisafishwa mara SABA (Zaburi 12:6)
32. Agano jipya imetaja tabia SABA za “heri”(Mt 5:3-9);
33. Neno “MIMI NI” lililosemwa na Yesu limetajwa mara SABA katika Injiri
(Joh 6:35; 8:12; 10:7, 11; 11:25; 15:7, 1),

Comments