JOSEPHAT MWINGIRA: JINSI NILIVYOTOKEWA NA BWANA YESU: AKIWA MBINGUNI MWINGIRA ANAONYESHWA JINSI MAPEPO YANAVYOFANYA KAZI PIA APELEKWA KUZIMU NA KUONA KILA KITU.(3)
BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.
Leo tunaendelea na sehemu ya 3 ya ushuhuda wa mtumishi wa MUNGU Josephat Mwingira, mbeba maono wa huduma ya Efatha yenye makanisa zaidi ya 200 hadi sasa. Kama hukusoma sehemu ya pili ambapo Malaika alikuja kumchukua Duniani na kumpeleka mbinguni FUNGUA HAPA
Leo tunaendelea na sehemu ya 3 ya ushuhuda wa mtumishi wa MUNGU Josephat Mwingira, mbeba maono wa huduma ya Efatha yenye makanisa zaidi ya 200 hadi sasa. Kama hukusoma sehemu ya pili ambapo Malaika alikuja kumchukua Duniani na kumpeleka mbinguni FUNGUA HAPA
Leo ni sehemu ya 3 ambapo akiwa mbinguni anapewa kazi na BWANA YESU na baadae anapelekwa kuzimu na baadae anaonyeshwa jinsi mapepo yanavyofanya kazi .
Karibu
KUSUDI LA WITO WANGU
1. Kuwafungua waliofungwa
2. Kuponya wagojwa na wenye misiba mbalimbali
3. Kuwafunulia watu siri za uzima wa milele
4. Kuwatayarisha watu tayari kwa kunyakuliwa. Katika
kuwatayarisha watu, kuna mambo ambayo alinieleza kufanya
5. Kuwaweka watu kwenye nafasi zao za utumishi. Yaani, kumpanga
kila mtumishi kulingana na wito uliopo ndani yake, kuanzia wito wa juu mpaka wa
chini, ili kila huduma isaidie kufikia kusudi la wito wake.
Napewa KUSUDI nililoitiwa
Akaanza kunieleza KUSUDI
aliloniitia. Akaniambia kuwa KUSUDI kubwa aliloniitia lilikuwa kunionyesha
mambo yote yanayohusiana a UUmbaji yalivyo.
Mambo ya Uumbaji yalivyo
Akanionyesha mambo ya Uumbaji
yalivyo kuanzia mwanzo, kama kitabu cha Mwanzo kinavyosema. Halafu akanionyesha
mwisho, kama kitabu cha Ufunuo kinavyosema. Akanieleza juu ya Kitabu cha
Ezekiel na Kitabu cha Daniel kinachozungumzia mambo ya kwanza na mambo ya
mwisho. Akanieleza jinsi mwanadamu alivyokuwa. Akanieleza habari za Luciferi na
jeshi lake linavyofanya kazi. Akanieleza mabo mengi mazito ambayo alitaka mimi
niyajue.
Nilipomuuliza kwa nini alikuwa
ananijulisha mambo yale mazito, akasema, “wewe utakwenda kuyafanya haya kwa
ajili ya ndugu zako!” na akaongeza kuniambia, “Wewe umejaliwa haya ili
ukayafunue huko, maana umejaliwa kuzijua siri za MUNGU, na umeamriwa kuzijua.
Sio wote waliojaliwa haya; lakini wewe umejaliwa kuzijua”. Halafu akaniambia
jinsi mwanadamu ambaye hajaokoka alivyo: hali kadhalika aliyeokoka anavyokuwa.
Yaani, akanionyesha moyo wa mwanadamu na mawazo yake – yaani mambo anayowaza.
Akanifundisha vitu vingi mno. Kitu kingine ambacho nakumbuka, alisema, “Kila
atayekusikia”, sasa haya aliyasema mwisho, “na atakayefanya utakachosema,
atajaliwa thawabu”.
Naonyeshwa kuzimu na BWANA YESU
Kutoka pale, akanipeleka kwenye eneo
linguine, akanipleka kuzimu ili nione kulivyo. Hilo lango la kuzimu lilifinguka
lenyewe. Akanionyesha, na mimi mwenyewe nikaona mafunza mkubwa kama ngumi.
Makubwa, halfu yana uwezo wa kuruka. Nikawasikia watu wanapiga kelele na
nikawaona wanalia kweli. Kuna giza kubwa sana huko, unawaona funza wanatoka
upande mmoja kwena ubande mwingine, wakiendea hao watu wanaolia. Wanapofika,
hata kama ni mgongoni, basi wanatoboa na kuingia kwenye migongo ya wale watu.
Baada ya hapo, unasikia wale watu wanapiga kelele sana kwa uchungu. Funza hao
wantoboa toboa kila sehemu za miili, na kila wanapotoboa, unasikia kelele za
hao watu wakilia.
Nikamuuliza BWANA YESU, “Hii ni
nini?” Akasema, “Ni mateso wanayoyapata watu huku kuzimu”. Nikauliza tena, “Je,
ina maana hii ndiyo itakavyokuwa adhabu yao mmilele?” Akasema, watakapopelekwa
katika Jehanamu ya moto, huko ndiko watakaa milele na milele”.
BWANA YESU ana ‘Nguvu’ isiyo ya
kawaida. Hakuna mahali ambapo hawezi kuingia. Usifanye mchezo, YESU ana nguvu!
Yaani hata kama ni mlango, mnapokaribia, kule kusogelea tu, mlango huo
unafunguka wenyewe. Yaani YESU ana Nguvu, hana cha mchezo. YESU ana Nguvu! Yaani
hata na mimi niliyashangaa sana niliyoyaona kule kuzimu kuhusu Nguvu zake.
Wakati tulipokuwa tunatembea kule kuzimu, tulipofika mahali na tulitaka kukaa
kidogo, tulikuwa tunaona kiti chake YEYE kimekwesha kufika na amekwesha kukaa,
hakuna mtu aliyekuwa anakileta. Na mimi nikaangalia kwa makini kile ambacho
BWANA YESU alikuwa anakifanya. Kumbe, nikaonyesha hali ya kutaka kukaa, nikona
kiti kimekwisha kufika, nikakaa!.
Baada ya hapo, tukaondoka na
kuelekea upande wa pili wa kuzimu, yaani katika eneo la lango la Jehanamu ya
moto. Huko nikaonyeshwa moto mkali unaowaka, ingawa hakukuwa na watu, kwa
sababu moto unasubiri siku ya mwisho. Katikati ya Jehanamu, kulikuw ana
barabara kubwa sana ambayo tuliivuka. Tukaondoka kutoka eneo hilo, na BWANA
YESU akanirudisha tena karibu na eneo la kuzimu. Hapo akalifungua lile lango,
akanionyesha Lucifer. Ndipo nilipomuona Luciferi akiwa anafanana nap aka
mkubwa. Kichwa chake kilikuwa kimepasuka mfano wa alama ya msalaba. Nikamuuliza
BWANA YESU, “Kwa nini kichwa cha Luciferi kimepasuka?” Naye akanijibu, “Hali
hii ilitokea saa tisa alasiri, siku ile pale msalabani, wakati lile pazia
lilipasuka. Tukio hilo, liliharibu kabisa mawazo ya Lucifari (shetani)” .
ukisoma katika kitabu cha wokorintho (2Kor. 10:4-5), Mtume Paulo anasema maneno
ya ajabu sana. “Silaha za vita vyetu si vya mwili, bali zinauwezo katika MUNGU
hata kuangusha ngome. Tukiangusha fikra na mawazo”.
Kuanzia siku ile, pazia lilipopasuka
pale msalabani, BWANA YESUalimshinda kabisa setani katika mamlaka yake na ufalme
wake. Ndiyo maana anatuambia alitupa mamlaka na ufalme. Yaani alimunyang’anya
shetani mamlaka yake na ufalme wake na kutupatia sisi. BWANA YESU akaniambia,
“Shetani hana kitu chochote anachoweza kumshindia mwanadamu. Anachofanya
shetani, ni kuwahi mawazo ya mwanadamu, na fikra zake, na nia ya moyo wake.
Akishafanikiwa kukamata mawazo, fikra na nia ya moyo wa mwanadamu, hana uwezo
wa kutenda jabo jingine lolote kwa mwanadamu kinyume na mapenzi ya MUNGU.
Naelezwa jinsi mapepo yanavyofanya kazi
Tukatoka sehemu ya Luciferi na
kwenda sehemu ya mapepo. Akanionyesha jinsi mapepo yanavyofanya kazi. Huyu
Luciferi, naye, anajeshi lake, lenye makundi mengi. Katika kuyahesabu, nikakuta
kuna makundi kama mia mbii na hamsini hivi. Kila kundi lina mamlaka yake, lina
utendaji wake, na lina nguvu zake.
Luciferi hakusema kitu.
Nilichoshangaa. BWANA YESU allinipeleka kwenye eneo lingine ambalo pia yako
mapepo. Yaliponion mimi na BWANA YESU, yakasujudu. Yaani, yaliinana kabisa.
BWANA YESU akaniambia, “Ndiyo yatakavyokwenda kutenda mbele yako! Yaani,
yataslimu amri mbele zako. Yatakuinamia”.
Nikaw anavishangaa vitu hivi na
mambo haya. Wakati tunamsogelea Luciferi, alikuwa mbali lakini katika ulimwengu
wa kiroho hakuwa mbali, alionyesha hali ya unyenyekevu, kama mtu ambaye
anaonyesha heshima ya kupita ‘Bwana Mkuwa’. BWANA YESU akanikumbusha Neno
lililoko kitabu cha Efeso (Efes. 6:11-14) linalosema, “Vita vyetu si juu ya
damu na nyama, bali ni juu ya ‘flme’ na ‘mamlaka’…”. Ukisoma pale utaona kuna
pointi za msingi tano. Zile pointi, ndizo zimegawanyika katika lile jeshi la
kipepo. Yamegawanywa katika makundi hayo mia mbili hamsini yenye majukumu
tofauti. Mengine yanapambana juu ya ndoa, mengine yanapambana juu ya watoto,
mengine yanapambana juu ya makabila ya watu, mengine yanapambana juu ya uchumi,
mengine yanapambana juu ya Watakatifu, na kadhalika. Kwa hiyo, usipoelewa
unapambana na mapepo ya aina gani, inakuwa taabu kuyashughulikia.
Mamlaka tatu
Tulipotoka pale, kwenye sehemu ya
mapepo, akanipeleka katika eneo ambalo linamazingira Fulani – kitu cha msingi
cha kufahamu ni kwamba shetani hatawali eneo linguine zaidi ya eneo la giza.
Hii dunia unavyoiona, imegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni
‘Utawala wa MUNGU’ ambayo unamilikiwa dunia nzima, na hata utawala wa ‘Mamlaka
yashetani’ uko chini ya hiyo mamlaka. Sehemu hii, tunaiita ‘Ufalme wa MUNGU’.
maana, pia, ili shetani afanye kazi vizuri, ni lazima aombe kibali kutoka
mamlaka hiyo. Halafu, kuna mamlaka ya Kishetani ambayo tunaiita ‘mamlaka ya
giza’ kasha, kuna ‘mamalaka ya wanadamu’ ambayo iko chini ya mamalaka ya
Uumbaji. Mamalaka hii tunaiita ‘Ulimwengu wa asili’. Mamlaka hii nayo, ina
utendaji wake na nguvu zake.
Lakini mamalaka zote ni za MUNGU.
Kati ya hizi, ni mamalaka mbili tu, mmlaka ya asili na ile mamalaka ya giza,
ndizo zinazoshindana. Mamalaka hizi zinashindana kwa sababu mamalaka ya giza,
yaani Lucifer, alinyang’anywa mamlaka yake, akapewa huyu mwanadamu. Sasa
Luciferi anapambana ili kumnyang’anya huyu mwanadamu mamlaka hiyo, akifanikiwa
kumlaghai. Luciferi anaweza tu kumteka mwanadamu pale anapofanikiwa kushika
mawazo, fikra na nia ya mouo wake. Hivyo, akishakamata mawazo ya mwanadamu,
anaweza kumfanya huyu mwanadamu afanye dhambi, yaani mambo ya giza. Kwa hiyo,
ikishafika hapo, mwanadamu anakuw akatika hali hiyo ya uovu na katika mazingira
hayo. Lakini asipokuballi kukamatwa katika yale mawazo, mwanadamu anabaki
katika mazingira yake, anatakiwa akubali kuenenda sawasawa na maandiko ya
Bibilia yanavyosema. Kwa kufanyahivyo, nia yake inakuwa ni nia ya MUNGU.
Mwanadamu, kwa ujumla, kabla hajakubali hilo, anaweza akawa hamjui MUNGU
kabisa, lakini nia ya moyo wake ikawa ya kutenda mema. Kwa hiyo anakuwa
hajakamatwa na huyu mfalme wa giza, ambaye ni Luciferi.
ITAENDELEAAAAA.....................
Usikose sehemu inayofuata hapa hapa Maisha ya ushindi blog pia unaweza kwenda Efatha na ukanunua kitabu hicho hapo chini ambacho ndio kina ushuhuda hu wote. MUNGU akubariki sana na endelea kutembelea hapa
Usikose sehemu inayofuata hapa hapa Maisha ya ushindi blog pia unaweza kwenda Efatha na ukanunua kitabu hicho hapo chini ambacho ndio kina ushuhuda hu wote. MUNGU akubariki sana na endelea kutembelea hapa
![]() |
WAKATI WA MKESHA EFATHA KIBAHA. |
Comments