JOSEPHAT MWINGIRA: JINSI NILIVYOTOKEWA NA BWANA YESU: AKIWA MBINGUNI MWINGIRA ANATOLEWA VIGAMBA MACHONI NA AWEZE KUONA ROHONI.(4)
Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira |
Leo
tunaendelea na sehemu ya mwisho ya ushuhuda wa mtumishi wa MUNGU Josephat
Mwingira, mbeba maono wa huduma ya Efatha yenye makanisa zaidi ya 200
hadi sasa. Kama hukusoma sehemu ya pili ambapo Malaika alikuja kumchukua Duniani na kumpeleka mbinguni FUNGUA HAPA
baada ya kutoka kuzimu, BWANA YESU alimuonyesha mambo mbalimbali ambaye tumeyaona katika sehemu ya 2 na ya 3 hapa sasa ni hitimisho na hapa kuna mambo makubwa zaidi ambayo BWANA YESU alimuonyesha Mwingira.
karibu.
Naelezwa siri ya mwanadamu
Baada ya kutoka sehemu ya mamalaka,
BWANA YESU alinipa siri ya mwanadamu. Alinieleza kuwa, mwanadamu kama
mwanadamu, ndiye mwenye uhalali juu ya dunia, na siyo shetani. MUNGU ndiye
aliyempa huu uhalali. Kwa hiyo MUNGU hawezi kumiliki dunia kwa maana anajua
kwamba amempetia mwanadamu, japo MUNGU andye muweza wa yote. Hivyo, mwenye
uhalali wa kutumia vya duniani na dunia yenyewe ni mwandamu. Mwenye faida na
dunia ni mwanadamu.
Tukiwa hapo, ndipo akanieleza juu ya
KUSUDI la kuniita mimi kwamba shetani hawezi kuitumia dunia kuharibu watu na
vitu vilivyomo, mpaka ampate mtu wa kumtumia. Sipofanya hivyo atakuwa amevunja
sheria ya Uumbaji ambayo inasimamiwa na MUNGU mwenyewe, MUNGU kama
MUNGU anaitwa MUNGU MKUU kwa sababu YEYE ndiye Mkuu wa yote na vyote vyenye
asili ya Ki-Ungu – kama Malaika na wanadamu- ambao waliumbwa ili wishi milele,
lakini kwa sababu ya ‘kosa’, haitakuwa hivyo tena. Hata kwa MUNGU pia,
utaratibu anaotumia, ni huo uo. Hawezi kuwa na uhuru wa kufanya kila kitu
duniani cha kumpinga au kumpiga shetani, mpaka ampate mtu atakayesimama kwa
ajili yake. Isaya (Isay 6:8) anasema alisikia sauti ya BWANA ikisema. “Nimtume
nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Ndipo BWANA YESU, pia, akaniambia
“Ninataka wewe, Josephat, uende ukafanye kazi hiyo”. Nikashangaaa sana.
Nikapokea UTUME kutoka kwa BWANA YESU”.
BWANA YESU,akasema,”Uhai wa
mwanadamu ni wa muhimu sana kwa upande wa MUNGU duniani. Yaani, uhai wa mtu
duniani, ni muhumu sana kwa MUNGU kuliko mtu huyo kufa. Uhai wa mwanadamu
unamfanya MUNGU aweze kufanya kazi kubwa zaidi na kupata tukuzo zaidi duniani.
Ndiyo maana, katika kitabu cha Kutoka (Kut 15:26), MUNGU anaagiza na kuahidi
kuwa, “Utaisikiliza kwa bidii sauti ya BWANA, MUNGU wako, na kufanya yaioelekea
mbele zake; mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa
mimi ndimi BWANA nikuponyae”. MUNGU, hata siku moja, hafurahii mtu akifa kabla
ya wakati wake au kabla ya kutimiza kusudi alilomwambia.
Majukumu niliyopewa.
Tulipotoka pale, akanionyesha eneo
linguine ambalo ni ‘Makao Matakatifu’. Baadaye, tulipomaliza kuzinguka,
akaniambia, “Sasa nataka urudi duniani”, maana alikuwa amekwesha nionyesha
mambo mengi, pamoja nay ale yatakayofuata baada ya ‘karamu ya Mwana kondoo’.
Kitu cha muhimu alichoniambia ni kwamba, alitaka mimi nirusi duniani
nikajiandae kwa ajili ya kazi ambayo ilikuwa mbele yangu. Na majukumu yenyewe
niliyopewa ni kama ifuatavyo:-
Huduma nilizopewa
Akanieleza juu ya tofauti ya Huduma
zile tano, zilizomo katika Kitabu cha Efeso (Efes 4:11) na katika Kitabu cha
Wakorintho (1Kor 12:28). Akanieleza, na tofauti zake, na uhusiano wake, na
mazingira ya utendaji kazi wake. Akaniambia, “Utawaweka watu kazini kama
nitakavyokuagiza”.
huduma ya kuhamishia
Akaniambia, “Nimekupa Huduma ndani
yako ya kuhamishia. “Pia, wakati huohuo, alinifanyia vitu kadhaa. Aliyashika
macho yangu, akatoa vigamba bigamba na kusema, “Kuanzia sasa, utaona mambo ya
Ki-Ungu. Mambo yaliyo katika ulimwengu wa roho. “Akanishika mikono na
kuambatanisha na mikono yake. Alipotoa mikono yake, nikaiangalia mikono yangu
nikaona damu. Akasema, “Nimeitakasa mikono yako, ili kila utakalolifanya,
likafanikiwe, na kila utakayemwekea mikono, akafunguliwe,” kasha kwenye macho
akaweka malaika, mmoja asimame upande huu na mwingine upande huu – walinde
macho yangu usiku na mchana, ili kuweza kuonanjia ya kwenda na kitu cha kufanya
kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili watu wake wanaokuja kwa ajili ya kumjua BWANA
. kasha akayagusa masikio yangu na kusema, “Kuanzia sasa, utaisikia sauti yangu
kwa usahihi. “Kwenye kinywa, akanifanyia kitu cha ajabu sana! Akaweka kidole
chake kinywani mwangu, akanigusa na kusema, “Kuanzia sasa Neno limetakaswa
kinywani mwako”.
Halafu akanishika miguu yangu katika
sehemu ya magoti na akasema, “Umetiwa nguvu miguuni na hata kwenye kiuno”
akaongeza kusema, “Utafanya kazi ambayo wengie hawajawahi kufanya”. Baadaye
akasema, “Kuanzia sasa, nimeweka mamlaka juu yako, na nguvu na uwezo.”
Akaniambia maneno mengi ya kunitamkia kwamba amenipa Huduma ya kuhamishia ya
‘Kitume’ na ‘Kinabii’. Akasema, “Katika utume wako, mwangalie sana Paulo
alivyopita kimamlaka, itafanana na hilo. Katika Unabii, angalia Isaya
alivyotabiri. Utatabiri mbambo yajayo, mambo ambayo hayajawahi kuwepo bado, wala
hayajawahi kutokea, wala hakuna aluewahi kuyatamka katika kizazi chako na
katika jamii yako, na yote yatatimia”. Akaniambia, “Uteweza kuwahudumia Mitume,
Manabii na wenye huduma zingine zote, kuwaweka kwenye nafasi zao”. Katika hilo,
akaniambia, “Nimmekupa upako wa kuhamishia ili wengine nao waweze kupokea”.
Akasema, “Ni wachache sana ninaowapa upako hii, kwa kuwa siyo wengi wana uwezo
wa kutumia”. Akaongeza kusema, lakini utakwenda kufanya kitu ambacho wengine
hawajawahi kufanya”. Akaendelea kusema, “Utakwenda kuweka nidhamu ya Ki-roho,
ambayo italifanya kanisa langu likue kwa kasi na kumshinda shetani. Nidhamu ya
Ki-roho ni pamoja na utendaji na utekelezaji”. Akaanza kunifafanulia kazi ya
zile Huduma nitakazokwenda kuzifanya.
Huduma za uponyaji
Katika Huduma ya uponyaji,
akanifundisha namna ya magonjwa yanavyokamata watu, na kutesa, na kadhalika.
Akasema, “Kila ugonjwa una chanzo , yaani, una asili yake”. Kwa hiyo, akawa
ananieleza asili ya kila ugonjwa. Nikauliza, “Sasa, mbambo gani yanasababisha ugojwa
gani?” YEYE akasema, “Vitu vingi”. Ndipo akanieleza ya kuwa, “MUNGU hafurahii
wagojwa. Hufurahia watu wakiwa na afya njema. Maana ndiyo aliyowapa. Bali, kwa
sababu ya uovu uliopo duniani, shetai amesambaza magojwa , lakini MUNGU ni
mponya
MUNGU wa mbinguni akubariki sana na asante sana kwa kusoma blog bora ya Maisha ya ushindi na jiandae pia kwa shuhuda mbalimbali ambazo watumishi wa MUNGU watashuhudia mahali hapa pia kama na wewe una ushuhuda wa kweli ambao MUNGU wa mbinguni amekutendea muujiza fulani, karibu kwa kushuhudia hapa maana kushuhudia ni kumwaibisha shetani , nitafute kwa namba hii 0714252292 au kwa email tumia mabula1986@gmail.com.
Efatha mwenge. |
Comments