KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ESA SALAAM LAANZISHA IBADA YA TATU SIKU YA JUMAPILI

mtumishi wa MUNGU Josephat Mwingira, mbeba maono wa huduma ya Efatha

Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa kanisa la EFATHA duniani na uongozi mzima waliamua kuanzisha ibada ya tatu ambayo itaanza saa 7:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni. Hii ikiwa ni jumapili ya kwanza ya 06.07.2014 ibada hii ilifunguliwa rasmi na mtumishi wa Mungu Nabii na Mtume Josephate Mwingira. Ibada hii inahusika na watu kutoka Sayuni, Yerusalemu na Amani.

Photo: Naibariki Jumatatu yangu...

Watu wengi waliokoka siku ya jana na kuyakabidhi maisha yao kwa Yesu Kristo. Kwahiyo ibada hii ilianza na mwanzo mzuri wa kuwavuna watu kwenda kwa Yesu Kristo. Waumini wa kanisa hili walifurahi sana na ratiba hii mpya, waliweza kuimba, kucheza na kumtukuza Mungu kwa vifijo na nderemo.

Ibada hii ilifungwa kwa kuiombea na pia kuibariki siku ya Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili siku ya mavuno.

Comments