KATIKA MLIMA WA BWANA ITAPATIKANA

 Na AP Hosea Shabani, Ufufuo na uzima Moshi, Kilimanjaro.
 
 
 
 
 
 
MWANZO 22:13-18

“............ Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana. Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”

Mungu alipomjaribu Ibrahimu amtoe sadaka mwanawe pekee Isaka, (mwana aliyempata kwa ahadi, mrithi na aliyempata akiwa mzee sana) na Ibrahimu bila kuyaangalia mazingira hayo na thamani ya mtoto huyo kwake akamtoa mwanawe Isaka mpaka hatua ya mwisho.
Mungu alikuwa anataka kuona moyo wa Ibrahimu kwake, na baada ya kuthibitisha kwamba hakika Ibrahimu ananipenda hata hawezi kunizuilia kitu chochote basi

Watu wengi tumekuwa tukitaka Mungu atende kama tunavyotaka na sio sisi tutende sawa na neno lake, tunataka neno la Mungu litufuate baadala ya kulifuata neno la Kristo. Tunapaswa kufahamu kwamba ili tumiliki malango ya adui zetu na Baraka hizi za Ibrahimu zitimie kwetu ni kwa kuenenda sawa na neno la Mungu kwenye maisha yetu na maadamu mtu ana imani kwa Mungu yuko tayari kutoa yale aliyonayo na kutii neno la Mungu sawa na neno lake.

Kwa kile alichokifanya Ibrahimu, kukubali kumtoa mwanawe Isaka ilimfanya Mungu aape kwa jina lake mwenyewe Mwanzo 22:15-16 “….Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, NIMEAPA KWA NAFSI YANGU ASEMA BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili”

Ibrahimu alikwenda kutoa sadaka katika kilima cha Bwana akapokea Baraka kuu mno, na yesu alikufa katika kilima cha Bwana nasi tukapata wokovu na leo upo katika kilima cha Bwana kwa kumtazama Yesu msalabani alipoangikwa unapata kile unachokihitaji nawe utamiliki malango ya adui zako na ushindi juu ya yote.

Ni habari njema kwako kwamba leo katika mlima wa Bwana Baraka zako zinapatikana, amani yako inapatikana, furaha yako inapatikana, ushindi wako unapatikana, kazi yako inapatikana na  Baraka zako zote kwa kumwamini mwana wa Mungu Yesu Kristo, nakila shida iliyokusumbua inakuacha huru sasa kwa kuwa wewe ni mwana wa Mungu unastahili Baraka hizi zote, kila shimo ulilochimbiwa liwanase wenyewe,  mawe waliyoyabilingisha yawarudie wenyewe uyamiliki malango ya maadui zako kwa jina Yesu wa nazareth. Amen.

Comments