KINACHOFANYWA NA NENO LA MUNGU KAMA LIKIKAA KWA WINGI MOYONI MWA MTU.



BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze somo hili ambalo MUNGU anataka tujue Matokeo ya Neno lake kama likikaa kwa wingi ndani yetu.

Yohana 8:31-32 inasema ‘’Basi YESU akawaambia wale wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu,  mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.’’
-        -Huwezi huwezi kuwekwa huru pasipo kweli.
-        -Neno la MUNGU linaweka huru.
-        -Tamani neno ambalo halijaghoshiwa.
-        -Watu hutenda dhambi kwa sababu kweli/Neno la MUNGU halimo ndani yao kwa wingi.

Katika Ayubu 22:21-22 Biblia inatufundisha jambo kubwa sana inasema ‘’ Mjue sana MUNGU ili uwe na amani, Ndivyo mema yatakavyokujia, Uyapokee tafadhali Mafunzo yatokayo kinywani mwake. Na maneno yake yaweke moyoni mwako.''
Hapa Biblia inatupa sababu za kumwamini MUNGU na pia sababu za kuyaweka maagizo yake yaani neno lake mioyoni mwetu.

Siku moja BWANA YESU alikuwa anatembea na wanafunzi njiani akaulaani mtu, wanafunzi wake wakashtuka sana na kwa sababu neno lake lilikuwa halijawakaa ipasavyo maana imani yao ilikuwa bado ndogo walihoji juu ya jambo hilo, BWANA YESU yeye aliwajibu kwamba ‘’Mwaminini MUNGU’’. Kumwamini MUNGU ni kitu muhimu sana na MUNGU analiangalia neno lake ili alitimize, itatuchanganya sana kama neno lake MUNGU tutakuwa hatulieweli.

KWANINI NENO LIMEBEBA HATIMA YAKO?

Ni kwa sababu MUNGU huliangalia neno lake ili atende jambo Fulani, na ili afanye kitu chochote kwetu huliangalia neno lake ambalo alikwishalitoa.

Isaya 55:11 MUNGU BABA anasema ‘’Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa sana katika mambo yale niliyolituma.''
-MUNGU atahukumu kwa neno.
-MUNGU atabariki kwa neno.
-Atasamehe dhambi kwa neno N.k


KINACHOFANYWA NA NENO LA MUNGU LIKIKAA KWA WINGI MOYONI MWAKO.

1.  Neno litakufanya usitende dhambi.
Zaburi 119:11 (Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. ).

2.  Neno litakufanya ujue hila za shetani. 
2 Kor 2:11 ( shetani asije akapata kutushinda kwa maana hatukosi kuzijua  fikra zake.)

3.  Neno hukutambulisha wewe ni nani na pia litakufanya ujijue wewe ni nani. 
Yohana 1:19-22(Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye KRISTO. Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? ).

4.  Neno hutakasa na kukufanya hai zaidi kiroho. 
Yohana 17:17 ( Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndio kweli.)

5.   Neno la MUNGU huleta tabia ya uungu. 
Zaburi 125:1 (Wamtumainio BWANA ni kama mlima sayuni ambao hautatikisika milele). MUNGU hatikisiki na mwenye neno lake hatikisiki. Utadumu  maana uko katika kweli ya MUNGU.

6.   Neno litakufanya kujua mpango wa MUNGU kwako Kumbukumbu 2:24 ( Ondokeni mshike njia……. Tazama nimewapa nchi hii muimiliki, anzeni kuimiliki,Mshindane nae katika mapigano)

7.   Neno la MUNGU litakufanya uwe na kiwango kikubwa cha imani. Yohana 20:5-16 ( Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia.
6 Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala,
7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.
8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini.
9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka.
10 Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao.
11 Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi.
12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.
13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.
14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu.
15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). )
             -Kiwango kidogo cha imani ni tatizo.
                    Wa kwanza akaona sanda.
                   Wa pili akaona sanda na leso.
                    Wa tatu akamwona YESU.
                    Wa imani akangoja na hatimaye akamwona BWANA.
 
Neno la MUNGU lingekuwa limewakaa wana wa Israeli wakati wakitoka misri naamini wasingeabudu ndama maana neno lingekuwa sababu yao ya kutokuabudu chochote zaidi ya MUNGU aliye hai, na hata kama mmoja wao angeshawishi wale wengine wasingelimsikiliza, hata Haruni angekuwa na ufahamu mzuri wa neno la MUNGU naamini angekataa kuwatengenezea ndama watu wale.


Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments