KURUDI KWENYE KUSUDI LA MUNGU LA MILELE

Na RP Adriano akifundisha ndani nyumba ya ufufuo na uzima Moshi
Kila mtu ana kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yake, ambalo ndilo limebeba maana ya yeye kuishi na ukiondoa kusudi unaondoa maana ya yeye kuishi na ukimuua mtu huyu unakuwa umeharibu kusudi.
Kutoka 4:19 “Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa.

Waebrania 11:23- “Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.”

Kwa imani Musa akakataa kuitwa mwana wa Binti Farao, Musa alikuwa anaongea kwa imani na iwe hivyo kwako leo kataa kuitwa maskini, kataa kuitwa tasa, kataa kuitwa mgonjwa, kataa kuitwa asiye na mbele wala nyuma na kila jina unaloitwa kinyume na makusudi ya Mungu kwa kuwa ulizaliwa kwa kusudi.

Baada ya kufa aliyeitafuta roho ya mtoto Yesu (Herode), Yusufu aliambiwa arudi na Musa pia walipokufa Farao na viongozi wake waliomtafuta aliambiwa arudi yaani akae akifanya anachotakiwa kukifanya, arudi kwenye makusudi ya Mungu na kufanya kile anapaswa kukifanya.
Watu wakisikiliza neno la Mungu alipokuwa akihubiri RP Adriano Ufufuo na uzima Moshi.
Tumeshambulia jana na kumumaliza anayetafuta maisha yako na yote uyafanyayo na sasa leo tuendelee mbele, hapo ulipo sasa KATAA KUONEWA, KATAA KUDHARAULIWA, KATAA KUIBIWA NA SHETANI MAWAKALA WAKE KWENYE MAENEO YOTE YA MAISHA YAKO KIMAFANIKIO, na mambo haya tunayakataa kwa imani yaani Rohoni nayo yanadhihirika katika  mwili.
 
Rumi 10:17” Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Tunakwenda makanisani kusikia neno na tunasoma neno kwenye mitandao imani yetu inajengwa na tunapata nguvu za kuharibu falme za giza na kurudi kwenye makusudi ya Bwana yale aliyotukusudia maishani
Maandiko yanaonyesha Israel walipokuwa utumwani walionewa na Mungu aliweka kusudi lake ndani ya Musa na shetani alipotaka kumuua Musa ililazimikia afe yeye ili makusudi ya Mungu yatimie ndani ya watu wake Israel.

Mwanzo 15:8-16 Maandiko yanaoonyesha kuwa hiki kilitokea kwa sababu ilikuwa ni makusudi ya Mungu, na Ibrahimu aliagana na Mungu mambo haya kwa hiyo isingekuwa rahisi kuharibu makusudi ya Mungu, na kwako pia Mungu ana makusudi ya kufanya kupitia wewe hutakufa na itafikia wakati watakuheshimu tuu maana itatokea bila wewe hawatafanikiwa kama ilivyokuwa kwa Yusufu walewale waliomfunga walimtoa ili awatafusirie ndoto, awatawale, awasaaidie.


Majeshi ya Platform yakimsifu Mungu ndani ya nyumba ya ufufuo na uzima Moshi

Tuombe pamoja maombi haya, “KWA JINA LA YESU KRISTO TUNAWAFYEKA WOTE WANAONIZUIA KUINGIA KWENYE MAKUSUDI YA MUNGU, WAFYEKWE MAJOKA NA WATAWALA WOTE WANAO ZUIA MAKUSUDI YA MUNGU KWENYE MAISHA YETU, KILA FARAO WA MAISHA YAKO NA AFE MWENYEWE KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH.

Katika jina la Yesu wewe ukaheshimiwe na waliokuonea wakitaka kusafiri wakute we ndo mtoaji wa visa, wakitaka kupona magonjwa yao wakakute we ndo mwenye dawa pekee ya shida yao, wakakuheshimu na Bwana akakuinue kati ya wote ukajazwe kicheko badala ya huzuni na ukafurahie makusudi ya Mungu kwako na yakatimie kwa jina la Yesu.

Amen.

Comments