KUTOKA KATIKA NCHI YA UTUMWA.

Na Snp. Mwangasa (Ufufuo Na Uzima, Moshi)
 Kutoka->14:13-14
“Musa akwaambia watu msiogope,simameni tu,mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo kwa maana hao wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.   BWANA atawapigania ninyi, Nanyi
Biblia inasema wana wa Israeli wakamlilia Musa wakiwa wamejaa hofu kuwa maisha yao  yataangamia,Musa alipokwenda kwa Mungu , Mungu akamwabia Musa usinililie mimi waambie wana wa Israeli wasonge mbele maana kesho asubuhi watakuwa nga’mbo ya bahari na hao Wamisri wanaowaona leo hawatawaona milele  ndipo Musa alirudi na kuwaambia wana wa Israli kuwa simameni mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia hivi leo,nayi mtanyamaza kimya bali Bwana atawapigania
                KUNA MABO MUHIMU YA KUJIFUNZA KATIKA SOMO HILI:-
             1) Israeli walikuwa kwenye jangwa hawakuona njia mbele yao ya kuwapeleka kwenye hatima yao,na maadui wanawafuata kwa nyuma ili kuwarudisha kwenye mateso ya jana ,Lakini pia Musa aliwaambia  tusonge mbele ili kueleke kesho yenye hatima yao.Musa alisisitiza kusonga mbele japokuwa mbele kulikuwa kuna bahari ya Shamu na hakukuwa na njia ya namna ya kuvuka lakini Musa alikuwa anajua Mungu anweza kufanya njia mahali pasipo na njia.
             2)Bahari ilionekana ni ngome ya ushindi kwa Wamisri  na kwa wana wa Israeli waliona bahari kuwa ni kikwazo Lakini kwa Mungu alikuwa anaona njia ndani ya Bahari na pia alikuwa anaona bahari kama mtego wa kuwaangamiza maadui wa watoto wake wana wa Israeli.
->Ndugu yangu  yawezekana leo na wewe upo kwenye jangwa la kimaisha umesongwa kila upande ni matatizo na maadui wamekuzunguka na vita ni vikali wala hauoni njia ya kutoka hapo na kushahuri Tulia kwa maana Bwana ameahidi kwenye neno lake Isaya->41:9-11”Wewe niliyekushika toka miisho ya Dunia na kukuita toka pembe zake,nikikuambia wewe u mtumishi wangu nimekuchaguwa wala sikukutupa Usiogope kwa maana mimi nipo pamoja na wewe usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako nitakutia nguvu ,Naam nitakusaidia, Naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu,Tazama wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika watu washindanao nawe watakuwa si kitu na kuangamia
              3)Israeli walipita mahali pa kavu katiati ya bahari na nyayo zao zilikanyaga mahali ambapo hapana  unyayo wa mtu mwingine uliwahi kupakanyaga
è Ndugu yangu yawezekana upo  kwenye shida au tatizo ambalo uzoefu wa kibinadamu  inaonyesha kwamba hakuna mtu aliyewahi kutoka katika shida au tatizo linalofanana na hilo ,Labda ni ugonjwa ambao madaktari bingwa wamesema hauna tiba,au  ni vifungo na watu wanakuambia aliyekuloga amekufa,
è Nina habari njema kwako leo kama utaamua kuchukuwa hatua ya Imani kwa kumuangalia Bwana Yesu  badala ya tatizo lako,Mungu atatengeneza njia ya kukutoa na kukupeleka kwenye hatima yako.
è Songa mbele nyayo zako zitakanyaga kwenye njia itakayokupeleka kwenye muujiza wa hatima yako,Hata kama kwenye familia  yenu,ukoo,kabila au jamii inayokuzunguka hakuna mtu aliyewahi kupita njia hiyo,Ni maombi yangu leo Bwana  Yesu akuwezeshe  wewe kuwa wa kwanza kupita katika jina la Yesu.
Watu wakiendelea kutoka nchi ya utumwa
           4)Musa aliwambia wana wa Israeli nyinyi mtanyamaza kimya bali Bwana atawapigania na kweli Israeli walishangaa vile kuona Mungu  anawatosa baharini Farao na majeshi yake  lakini wakati  Mungu akiwa anawapigania wao walikuwa wanasonga mbele kuelekea kwenye hatima yao.
è Ndugu yangu unapomuomba Mungu akupiganie au kukushindia vita wewe songa mbele ,usikae sehemu moja wala usirudi nyuma.
è Tambua kuwa kuna jana ,leo,na kesho Kimsingi wewe unaishi leo ili uitengeneze kesho yako  na ni vizuri kutambua   shetani yuko nyuma yako ili akurudishe kwenye shida zako za jana,kushindwa kwako kwa jana na mahangaiko yako ya siku za nyuma,Lakini pia tambuwa kuwa Bwana Yesu yuko msalabani mbele yako  anakuita umwangalie yeye na kusonga mbele
è Usiiangalie jana yako imepita bali macho yako ya Imani  yakupeleke kusonga mbele,Kesho yako imehifadhi muujiza wa hatima yako.
è Isaya 43;18-19 “Msiyakumbuke mambo ya kwanza  wala msiyatafakari mambo ya zamani tazama nitatenda neno jipya;Sasa litachipuka;je! Hamtalijua sasa?Nitafanya njia hata jangwani na mito ya maji nyikani”
Watu wakiombewa
       *Ni maombi yangu kwa Mungu leo Akuwezeshe kuchukuwa hatua ya Imani,na Ukatae kuwa mtumwa wa  utu wako wa kale na usonge mbele
*Kama wewe ni mgonjwa umelala kitandani au upo mahali popote chukua hatua ya Imani sasa maana Bwana yupo tayari kukupigania na kukushindia yote yanayokusibu ktika jina la Yesu Kristo,Anza kumshukuru Munfgu ukisema  Yesu asante kwa kupigwa kwako maana mimi nimepona
*Na kama wewe umefungwa kwenye laana,balaa,mikosi,nuksi,umaskini au tatizo lolote lilokuelemea ,Tamka maneno ya Imani kinyume na matatizo hayo ukitumia jina la YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU!

Comments