KWANINI TUHAHITAJI TUOMBE?


Mungu anatuhitaji tuombe, tunatakiwa tuombe sio tu kwasababu tunauhitaji bali kwa sababu Mungu anahitaji tuombe. Tatizo la watu wengi wanashindwa kupokea majibu ya maombi wanayoomba na wengine wameshindwa hata kuomba.wengine wamejikuta wakikata tama bila kujua kuwa wao ndio wanakosea katika kupeleka haja zao kwa Mungu na katika kupokea. Hapa
tutajifunza sababu na jinsi ya kuomba ili kupokea kutoka kwa BWANA.
SABABU NNE: KWANINI TUNAMUOMBA MUNGU:
1. Kujinyenyekesha mbele za Mungu.
2. Kuonyesha kuwa yeye ni Mungu wetu.
3. kuonyesha kuwa vyote viko mikononi mwake
4. Tunampa heshima kama baba mwenye familia ya watoto watakatifu.
MAOMBI YANAHUSISHA VITU VIKUBWA VITATU:
1. Mhusika AU muombaji mwenyewe:- huyu ndiye muombaji na mwanzilishi wa maombi.
2. Maombi yenyewe:- haya ni mahitaji au ujumbe ambao unapelekwa kwa unaye muomba.
3. Unayemuomba: - unayemuomba ni nani kwako na mna uhusiano gani naye. Kwa kujua umuhimu wa kuomba, wanafunzi wa Yesu walimwomba Yesu; awafundishe jinsi kuomba na hapo Yesu aliwapa fomula ya kuitumia ili kuomba.Hii ndiyo inayoitwa sala ya BWANA,
kimsingi hii ni kanuni ya kuomba aliyoifundisha Yesu na si maombi yenyewe kama wengi wanavyodhani,
KANUNI hii ni sawa na kanuni yengine za kufanya jambo fulani. Mfano kuna kanuni za kupika au kanuni za kuimba. Tatizo la watu wengi ni kwamba wanatumia hii kanuni kama ndio maombi yenyewe. Kwa mfano Yesu aliposema “Baba yetu uliye mbinguni…”alimaanisha kuwa unapokuwa unaanza kuomba ni lazima ujue unamuomba baba aliye mbinguni na si magomeni. Hii ni kanuni jinsi ya kuomba na haitaji moja kwa moja haja yako, bali ukiitumia kama
kanuni inakuletea majibu: =
Yakobo 5: 15-16 “kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii”, Biblia inaposema kuomba kwake mwenye haki: anamaanisha kuwa yeye anayeanzisha maombi ni lazima awe ni mwenye haki yaani msafi. Kiukweli kuna wakati mwingine Mungu hutenda
kwa sababu ya neema yake lakini kimsingi ili maombi yako yafae inabidi uwe mwenye haki. Hivyo kabla ya kuingia kwenye maombi unatakiwa ujitakase kwanza ili Mungu akikutazama
aone uko safi. Ni muhimu kutengeneza uhusiano mzuri na Mungu, tengeneza
haki kwanza kabla ya kuingia kwenye maombi. Yaani kama hujaokoka uokoke
kwanza, na kama umeokoka lakini hauko sawa na Mungu, unatakiwa utengeneze
maisha yako kwanza. Katika mstari wa 15* Biblia inasema “ungameni dhambi
zenu ninyi kwa ninyi” ikiimaanisha kuwa kabla ya kuingia kwenye maombi
unatakiwa ujisafishe na ujitakase kwanza. Baada ya kujitakasa kinachofuata ni
kupeleka ujumbe wenyewe kwa Mungu.Watu wengi kwasababu hukosea kuomba
wamedhania kuwa Mungu huwa hajibu maombi; lakini Biblia inasema Mungu
anajibu maombi. Biblia inasema, Zaburi 2:8 “uniombe nami nitakupa mataifa
kuwa urithi wako...” na katika Mathayo 7:7 “Ombeni nayi mtapewa…” kumbe
unapoomba lazima Mungu akujibu kama ukiomba sawasawa na mapenzi yake. Ni
muhimu kabla ya kupeleka hoja yako uamini kwanza kuwa Mungu yupo sawasawa na Waebrania 11:6 “...lazima aamini kuwa Mungu yupo”. Haya maandiko tutatumia katika kuangalia jinsi ya kuomba na wapi watu wengi wanapokosea wakiwa katika kuomba…
KANUNI ZA KUPOKEA KUTOKA KWA MUNGU:
Watu wengi wanajua kuomba lakini kati yao wengi hawajajua namna ya kupokea.
Kwasababu kuna namna ya kuomba na namna ya kupokea. Watu wengine wanajua kuomba lakini hawajui jinsi ya kupokea haja zao. Haifaidii kitu kujua kuomba na huku ukiwa hujui jinsi ya kupokea. Kuna mambo kadhaa ambayo unatakiwa uyatilie maanani unapokuwa unaomba kama ifuatavyo:-
1. Tengeneza uhusiano wako na Mungu:-Maandiko yanasema “haja zenu na zijulikane mbele za Mungu” pamoja na kuwa Mungu anajua haja zetu lakini bado anahitaji sisi tumuombe. Hii ni sawa na kuomba kwa jirani wakati baba yako mzazi yupo; utajisikiaje mtoto wako anapokuwa na shida alafu akuombi wewe baba yake, alafu yeye anajitengenezea sanamu na kuiomba. Utakavyojisikia ni sawa kabisa na Mungu anavyojisikia kwetu ndio maana Mungu anasema kuwa anaona wivu (kutoka 20:4). Mungu anataka tumuombe yeye ili kujenga uhusiano na yeye. Ukiomba au kuiabudu sanamu unamfanya Mungu
awe na wivu.
2. Unaongea nini ukiwa katika maombi yako:- Maombi unayoongea kwenye maombi ni ya muhimu sana kwenye kupokea haja zako kutoka kwa BWANA. Tuangalie kwa habari ya Hana; 1Samweli1:1-24; Elikana alikuwa na wake wawili Penina na Hana, kama lilivyojina lake Hana hakuwa na watoto kwasababu tumbo lake lilikuwa limefungwa. Hana hapo kwanza alikuwa anaenda na malalamiko na kulia. Watu wengi hupeleka malalamiko kwa BWANA, badala ya kupeleka hoja kwa Mungu.Hata siku moja Mungu atendi jambo bila kusudi, na ndio maana tumbo la Hana lilikuwa limefungwa kwa muda wote ule.Hebu tuangalie mambo kadhaa
yaliyokuwa yakimzuia Hana.>Sababu ya kuomba:-1Samweli 1:1-24 Hana alikuwa anamuomba Mungu ampe mtoto ili amkumeshe penina, na ndio sababu inayowafanya wengi washindwe kupokea kwa BWANA kwasababu hawana sababu ya Kibiblia inayowafanya Mungu awape
mahitaji yao. Mfano mtu anamwomba Mungu mke ili amfulie nguo au amechoka kuishi mwenyewe. Hiyo si sababu; Mungu anahitaji hoja yenye nguvu ili upokee mwambie jukumu lako la kutimiza kwenye maisha yako na nafasi ya mke katika kumtumikia Mungu;
hapo lazima akutendee.>Peleka haja ya moyo wako:-Mungu haitaji hali yako ikoje sasa bali
anahitaji kujua unataka nini. Picha ya tatizo lako unatakiwa uwe nayo wewe lakini mbele za Mungu unatakiwa upeleka haja ya moyo wako na si malalamiko. Kwa wakati ule Hana alikuwa anapeleka hali yake ilivyo na penina na si uhitaji wake kwa BWANA. Unakuta mtu anamuomba Mungu gari ili awaonyeshe wengine, huyo hawezi pata kwasababu si sawa na mapenzi ya
Mungu.>Mwangalie Mungu na si jambo unalohitaji: Ibarahimu alipompokea Isaka
ilimradhimu Mungu kumjaribu ili ajue upendo wake upo kwa Isaka au kwa Mungu. Watu wengi wanamuomba Mungu jambo lakini wakilipokea ndilo linalofanyika mzigo mkubwa wa kutokumtumikia Mungu, mfano mtu anaomba mume akipokea tu; baada ya siku chache haji kanisani anasema eti anamuhudumia mumewe. Kwasababu hii hata Hana akupata mtoto mpaka
alipobadilisha maombi na kumuomba Mungu mtoto, kwa kumuahidi BWANA
kumtoa mtoto huyo awe mtumishi wake.
3. Imani na Bidii: Watu wengi wanafikiri bidii ni kutumia nguvu tu katika maombi, bali bidii ni ule mzigo; ni muhimu unapokuwa unaomba uwe na mzigo wa kuombea. Ili uzae matunda katika maombi ni lazima uwe sawa na mama mjauzito aliye katika kuzaa; lazima uwe na uchungu yaani
umaanishe. Vivyohivyo kupokea kutoka kwa BWANA Unatakiwa umaanishe na lazima uamini pia kuwa ni wakati wako wa kupokea kutoka kwa BWANA. Unapoomba unatakiwa moyo na akili yako iwe kwenye kile unachohitaji. Kuna watu wanabidili maombi kila kukicha kwa
kuhisi kuwa Mungu awasikii lakini bidii ni kubaki kwenye jambo hilo hadi uone amani moyoni kuwa BWANA ameshatenda na hili jambo ndilo ambalo Eliya alilifanya alipokuwa anaomba mvua kunyesha tena. Eliya alikuwa mwanadamu wa namna moja na sisi alikuwa na Bidii katika maombi.
JAMBO LA KUFANYA:
Baada ya kujua mambo haya ni muhimu kubadili mtazamo wako na jinsi unavyoomba. Mungu anajibu maombi kama ukiomba sawasawa na NENO lake.Kwanza uwe na picha ya kile ambacho
unataka BWANA akutendee, uombe na imani na bidii. Hapo lazima Mungu akutendee kwasababu hakuna baba ambaye mwanaye atamwomba mkate akampa jiwe au samaki akampa nyoka. Badili mtazamo wako katika maombi yako ili uwe mpokeaji wa maombi yako ni si mwombaji asiyepokea chochote!!!

ambalo Eliya alilifanya alipokuwa anaomba mvua kunyesha tena. Eliya alikuwa mwanadamu wa namna moja na sisi alikuwa na Bidii katika maombi.
JAMBO LA KUFANYA:
Baada ya kujua mambo haya ni muhimu kubadili mtazamo wako na jinsi unavyoomba. Mungu anajibu maombi kama ukiomba sawasawa na NENO lake.Kwanza uwe na picha ya kile ambacho
unataka BWANA akutendee, uombe na imani na bidii. Hapo lazima Mungu akutendee kwasababu hakuna baba ambaye mwanaye atamwomba mkate akampa jiwe au samaki akampa nyoka. 


MUNGU akubariki sana .
By Faith Kaingu.
 

Comments