MAMBO MENGINE YATAONDOKA KWA KUAMURU TU.

 Na Nyandula Mwaijande
Bwana Yesu Asifiwe!
Leo tutafakari juu ya uweza wa Jina la Yesu Kristo!
Ndugu zangu si kila tatizo/shida uliyonayo itaondoka kwa maombi - bali nyingine zinaondoka kwa KUAMURU katika jina la Yesu Kristo shida hiyo iondoke au kwa KUAMURU hali unayoitaka itokee.


Badala ya kusubiri Mungu afanye kitu kwanza juu ya tatizo/shida hiyo, unaamuru shida hiyo iondoke na Mungu anasimamia utekelezaji wake.
Matendo ya Mitume 3:6-8
Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilichonacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, kumsifu Mungu.


Ndugu zangu iko nguvu itendayo kazi katika kulitumia jina la Yesu Kristo hivyo kama alivyolitumia Petro kuamuru yule kiwete asimame ndivyo na sisi hii leo tunaweza kufanya hivyo kwa kuamuru tatizo/ shida uliyonayo iondoke na ikatokea kwa sababu tumepewa mamlaka kwa jina la Yesu Kristo lenye uwezo usiobadilika.


Tuendelee kutafakari ujumbe huo na kuufanyia kazi hakika tutamshuhudia Mungu siku zote za maisha yetu.
Nawatakia jumatatu njema yenye ushindi dhidi ya shetani.

By   Nyandula Mwaijande

Comments