![]() |
Joseph Nyuki. |
BWANA YESU asifiwe sana.
Siku 3 zilizopita mtumishi wa MUNGU na mwimbaji wa nyimbo za injili Joseph Nyuki alitoa taarifa ambazo ziliwashitua sana wana injili popote walipo na aliwataka kuomba pamoja na yeye kwa ajili ya Mke wake.
Hata mimi jambo hilo lilinigusa sana na kwa maombi ya watumishi wa MUNGU na wana injili wote BWANA ametenda muujiza, jana mgonjwa ametolewa ICU na sasa yuko kwenye Wodi ya kawaida.
Ni jambo la kumshukuru sana MUNGU wa uzima kwa uzima wake.
Hii hapa taarifa ya Joseph Nyuki akiwashukuru walimwombea mke wake.
''Baada ya maombi yenu watu wa Mungu sasa mtumwa wa Bwana ametoka ICU yupo wodi yakawaida madaktari wamepambana sasa
Mke wangu anaendelea vizuri asanteni kwa kunitia moyo''
![]() |
Mke wa Joseph Nyuki akiwa kwenye wodi ya kawaida baada ya kutolewa ICU. |
![]() | |
Mke wa mbimbaji nguli wa nyimbo za injili Joseph Nyuki akiwa ICU. |
Habari ya mwanzo ni hii FUNGUA HAPA
Comments