MTALII KUSHTAKIWA KWA KUACHA BIBLIA HOTELINI

Rais Kim Jong Un na wasaidizi wake. ©Reuters/KCNA via CP
Kati ya mambo ambayo yanaisumbua jumuiya ya kikristo duniani basi ni mateso wanayoyapata maeneo mbalimbali, kuanzia Suda, Nigeria, Korea, Pakistan na sehemu nyingine nyingi kutokana na imani yao.

Huko Korea ya Kaskazini, mwanaume mmoja ameshikiliwa kwa tuhuma za kuacha biblia kwenye chumba cha hoteli yake, tofauti na maelezo ya alichokuja kufanya nchini humo (utalii).

Tukio hilo ambalo ni gumu kuelezeka masikioni mwa wengi linadhihirisha namna ambavyo taifa hilo linaloongozwa na Rais Kim Jong Un linavyowanyima watu uhuru wa kuabudu, kama ambavyo imeelekezwa kwenye kifungu namba 18 cha azimio la haki za binadamu (Universal Declaration of Human Rights) ya Umoja wa Mataifa.

(Everyone has the right to freedom of thought, conscience and religion; this right includes freedom to change his religion or belief, and freedom, either alone or in community with others and in public or private, to manifest his religion or belief in teaching, practice, worship and observance.)

Korea Kaskazini inafahamika kwa matukio ya namna hii, ambapo mtu yeyote anayejihusisha na injili hujiweka matatani, (ikiwemo tukio la hivi karibuni la Rais Kim kuagiza wakristo 33 kunyongwa)  ambapo Jeffrey Fowle amewekwa kizuiani kwa ajili ya kushtakiwa kutokana na kuhisiwa kueneza injili, tofauti na lengo lake la kutembelea nchi hiyo kama ilivyoelekezwa kwenye kibali chake cha safari (visa).

Hata hivyo familia ya Bwana Fowle kupitia msemaji wake imeeleza kwamba Jefreyy hakwenda huko kwa mrengo wa kuhubiri injili, ila kutembea tu.

Christian Post | Umoja wa Mataifa

Comments