Skip to main content
MTU ANAYEKUPENDA ATAKUJALI KWA KADIRI YA UWEZO WAKE, ATAKUTHAMINI KWA KADIRI YA UWEZO WAKE, ATAKULINDA KWA KADIRI YA UWEZO WAKE!
Hii alama iko wazi sana tukiihusisha na maisha yetu katika kujua
ukweli wa hiki nikisemacho! Na mambo haya hayakwepeki kufundishana na
kukumbushana! Kwasababu, upendo unatenda kazi sehemu zote; kwa marafiki,
ndugu na kwa sehemu tulizozizoea!
Kitu unachokipenda huwezi kukiweka ovyoovyo, huwezi kukiweka mahali popote, wakati mwingine huwezi kumruhusu
mtu yeyote tu akitumie au hata kukishika! Na zaidi sana utakuwa
muangalifu wakati wote kwa kukijali na kukitunza, utakuwa makini sana
katika kukilinda!
 |
Na Marko Bashiri |
Ndivyo
inavyokuwa kwa mtu unayempenda au anayekupenda, atakujali sana kwa
kadiri ya uwezo wake! Nasema tena " Atakujali na kukutunza na kukulinda
kwa KADIRI YA UWEZO WAKE.." Kujali kunaambatana na mambo mengi!
Kunaambatana na kusikiliza na kutii! Kama mtu anaongea halafu wewe
unakuwa unafanya mambo yako; huko sio kumjali mtu! Hizo ni dalili za
dharau, ndio maana ni rahisi kusikia " Mi naongea yeye wal hata ajali
anafanya mambo yake..." Ile hali ya kusikiliza kwa kile mwingine
anachosema au kuzungumza, huko kunaonyesha kujali na ndio moja ya alama
muhimu ya upendo! Kumjali mtu sio lazima uwe na pesa! Ni kwa kadiri ya
uwezo wa mtu! Maana wako watu wanatoa pesa na hawapendi wala hawajali!
Ni kwasababu pesa zipo na hana choyo au amezoea kuhonga anatoa tu! Ili
apate anachokitaka au aendeleza anayoyataka lakini ndani mwake hakuna
upendo wowote ule! Anayekupenda atakuthamini, atakuweka katika daraja la
juu sana na kukutunza na kukulinda! Yote hayo atayafanya kwa kadiri ya
uwezo wake, atakutunza kwa kadiri ya uwezo wake! Haitowezekana yeye avae
vizuri huku anakuangalia wewe huna chochote, labda kama mwingine
hapendi anapenda kuwa kawaida! Haiwezekani yeye ale vizuri huko kwenye
mizunguko yake halafu wewe huku unakula chakula cha shida au unakula
chakula cha siku iishe wakati yeye anakula vinono! Anakulia hotelini
akija huko anajifanya hali sana, kumbe ameshakula vinono!
Mtu
anayekupenda kweli! Atakuthamini, atakutunza na kukulinda katika vipindi
vyoote kwa kadiri ya uwezo wake, ukiwa kitandani hujiwezi kwasababu ya
kuugua, atakujali, atakuthamini, atakutunza na kukulinda pamoja na
kutapika kwako yeye haoni kinyaa, ndio kwanza atahakikisha unakuwa
msafi! Upendo ndivyo ulivyo, haihitaji kulazimisha! Upendo ndivyo
ulivyo!
SHARE na marafiki zako!
By Marco Bashiri
Comments