MWANADAMU HAWEZI KUWA MPELELEZI WA MUNGU.

 Na Kabalama Masatu

Nakusalimu katika jina la Yesu jina lile lipitalo majina yote.
Karibu sasa tujifunze pamoja somo hili liitwalo "MWANADAMU HAWEZI KUWA MPELELEZI WA MUNGU".
Katika kitabu cha Mithali20:27 tunasoma:-
"Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA;Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake".
Oooh, Alleluyah!
Hebu labda tuangalie haya maneno, "Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana".

Kazi ya taa ni kumlika mahali fulani na kufanya kila kilichopo mahali pale kiweze kuonekana.

Kumbe kama ndivyo, basi pumzi yako/yangu ndiyo inamwezesha Bwana kuona kilichomo ndani yako,kuona unawaza nini.
Maana pale unapopumua tu kila kitu kinakuwa wazi mbele za Bwana.
Sasa jambo hili watu wengine wanashindwa kulielewa hivyo hawaweki hofu kwa Mungu badala yake wanaweka hofu kwa wanadamu.
Nadhani sasa tunapasa kutambua ya kuwa hakuna lolote ambalo mwanadamu atalifanya kwa kuwaficha wanadamu halafu wakati huo huo akidhani ya kwamba amemficha na Mungu.
Hili ni jambo la ufinyu na upungufu wa mafundisho yenye kuwaongoza watu katika kweli.
Wapo watumishi waliojingea mazoea ya kuabudiwa na kunyenyekewa utadhani wao ndio wanapeleka taarifa kwa Mungu(wamejiweka kuwa wapelelezi wa Mungu).
Lakini ndugu yangu utambue yakwamba haina haja ya kufanya mambo kwa siri eti tu wapendwa wengine wasikuone.
Hilo halisaidii chochote na tena halitakuokoa maana kila kilichomo ndani yako kiko wazi mbele za Bwana kwa sababu pumzi yako ndiyo taa yake.
Utaendelea kutenda mambo yako yasiyompendeza Bwana kwa siri mpaka lini?
Ooooh,mpendwa naona uchungu sana kwa ajili ya roho yako.
Napata shida sana kwa ajili ya mahali pale utakapokuwepo baada ya kuiacha dunia hii.


Sheria za wanadamu haziwezi kukuokoa,mapokeo ya dini hayawezi kukuokoa;Ila ni Yesu pekee.
Ukimpata huyu Yesu umepata yote,taarifa zako zinakuwa safi mbele za Bwana.
Fanya maamuzi ya kuijua kweli.


 Mithali20:27 imeandikwa:-
"Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA;Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake".


Kumbuka tuliangalia kazi ya taa kwamba ni kumlika mahali pa giza na kuwezesha kila kitu kionekane kwa urahisi.
Sasa hili ndilo ambalo Suleiman anatuambia kwamba "ni taa ya Bwana tena inapeleleza kila kitu kilichomo ndani yake".
Ndiyo;Suleiman anatambua vizuri kwamba Bwana anajitoleza yeye mwenyewe kufanya upelelezi na siyo mwanadamu ndiyo afanye kazi hiyo.
Anachotambua ni kwamba mwanadamu atapeleka taarifa zisizo za kweli hivyo Mungu akajiwekea utaratibu wa kupata taarifa zote za wanadamu kwa kuweka pumzi yake mwenyewe ili kupitia pumzi hii basi taarifa zote zimfikie yeye.
Sasa hawa wanadamu wanaojitia wapelelezi wa Mungu ili tuwaabudu wametoka wapi?
Wana nafasi gani kwa Mungu?
Kumbuka jambo hili mjoli wa Bwana mtumishi kuwa na upako siyo ndo tumwabudu.Upako hauwezi kuokoa ila Yesu Kristo ndo anaokoa.


Kumbe unapasa kumwabudu Mungu tu ndani ya Yesu Kristo na kuwa na hofu mbele za Mungu wala siyo mwanadamu.
KUMBUKA:Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huzipima roho za watu.Mithali16:2.


                                           *MWISHO*.
Mawasiliano ni:
0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments