MWANAMKE SUDAN AFUNGULIWA KESI MPYA NA NDUGU ZAKE WAKIDAI NI MUISLAMU NA SI MKRISTO




Ndugu wa mwanamke aliyepona kunyongwa kwasababu ya kukataa uislamu Meriam Ibrahim amefunguliwa kesi nyingine juzi alhamisi na ndugu zake ambao wamedai kwamba mwanadada huyo ni mwislamu na si mkristo kama anavyodai mwenyewe.

Kwa mujibu wa mwanasheria aliyelipwa na familia ya ndugu wa Meriam aitwaye Abdel Rahman Malek amesema mahakama inayojihusisha na mambo ya dini ya jijini Khartoum itaangalia upya kesi ya Meriam kujiridhisha na ushahidi ambao ndugu zake watautoa dhidi yake kama kweli bado anahusiano wa kifamilia na baba yake. Kitendo cha kufunguliwa kesi mpya dhidi ya Meriam kunafanya juhudi zao za safari ya kwenda Marekani pamoja na watoto wao itachelewa.

Aidha kwa upande wa wakili wa Meriam aitwaye Mohamed Mustafa amesema mteja wake bado hajapewa taarifa za kufunguliwa kesi hiyo na ndugu zake upande wa baba yake kwakuwa familia hiyo anatambulika kama Meriam Abrar ikimaanisha anatumia jina la Abrar al-Hadi Mohamed Abdalla. Mustafa amesema bado haijajulikana kesi hiyo itasikilizwa lini lakini pia anatumaini mahakama itatupilia mbali shitaka hilo.

Kwa mujibu wa Christian Post wameandika kwamba Meriam alizaliwa katika familia ya baba muislamu ambaye aliitelekeza familia toka Meriam akiwa mdogo hivyo kulelewa na mama yake muethiopia ambaye ni mkristo wa dhehebu la Orthodox na kwamba toka wakati huo Meriam amekuwa akitambulika kama mkristo katika maisha yake yote.

Comments