NEEMA GOSPEL KWAYA NDANI YA MAJONZI MAZITO YAKUONDOKEWA NA MWENZAO


Marehemu Mandilindi William enzi za uhai wake akiwa jijini Nairobi nchini Kenya walipokwenda kihuduma na kwaya yake ya Neema gospel.

Kwaya ya Neema Gospel ya kanisa la AIC Chang'ombe jijini Dar es salaam, imepata pigo la kuondokewa na mmoja kati ya wanakwaya wao aitwaye Mandindi William aliyefariki jana jioni katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa wanakwaya wa kwaya hiyo kupitia ukurasa wa Facebook wa
Mandi kushoto akiwa na wapigaji wa Neema gospel.
kwaya hiyo amesema wakati wakirekodi cd mpya ambayo wameizindua jumapili iliyopita, kijana huyo aliwaambia wenzake kwamba anaumwa inni akizungumza kwa utani ambao hata wenzake hao waliishia kucheka.

Marehemu Mandilindi alikuwa mmoja kati ya vijana watatu wa kwaya hiyo ambao wanavipaji katika kuanzisha nyimbo akiwemo Samuel Limbu, Charles Izengo pamoja na marehemu ambaye kupitia sauti yake ya upole ambayo unaweza kuisikiliza kupitia wimbo wa 'Ponya kanisa lako' ulioimbwa na kwaya hiyo ambapo kijana huyo anaimbisha kuanzia dakika ya 6 na sekunde ya 22 akiimba 'Bwana ni nuru yetu nani tumhofu…' imewabariki wengi waliosikiliza na kutazama wimbo huo.

Mandilindi wa kwanza kuume akiwa na wenzake ambao kwa pamoja walikuwa wakiitwa mapacha watatu kwa kazi yao njema katika kumuinua Kristo.
  Tunatoa pole kwa Neema gospel kwaya, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba wa mwinjilisti katika huduma ya uimbaji marehemu Mandilindi William.

                            credit:Gospel Kitaa

              Mtizame marehemu akiimbisha wimbo huu kuanzia dakika ya 6 na sekunde 22.


Comments