NEEMA JUU YA NEEMA.

Na. Hossea Shabani, UFUFUO NA UZIMA MOSHI, KILIMANJARO.


Watu wote tumeokolewa kwa neema ambayo haikutokana na matendo yetu mazuri, au kwamba tulitoa vitu vya thamani sana hata Mungu akatupa wokovu sisi. Mambo haya hayamaanishi kwamba wengine wote ambao hawajapata wokovu na kubakia katika utumwa wa shetani.
Na maandiko yanasema katika Yoh 1:1-16.
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.……….. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; AMEJAA NEEMA NA KWELI. Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. KWA KUWA KATIKA UTIMILIFU WAKE SISI SOTE TULIPOKEA, NA NEEMA JUU YA NEEMA.”

Mungu mwenyewe aliamua kutuokoa kwa neema, TUKAPOKEA NEEMA JUU YA NEEMA, hatukustahili wokovu huu tulionao lakini Mungu kupitia mwanawe akaamua kushuka chini akavaa mwili akaamua kutuokoa kwa namna ya ajabu. Na baada ya kuipata neema hii Mungu anatutaka tuishirikishwe kwa wengine ili na wengine pia waweze kuipata neema hiyo.

Tutambue kwamba sisi si BORA kuliko wengine, na tukishatambua kwamba sisi si bora kuliko wengine tutathamini neema tuliyoipata na kuchukua hatua za makusudi kuihubiri kwa wengine ili nao wapate, maana hata sisi pia tuliisikia neema hii kutoka kwa waliotutangulia na hata tukapata kuamini na vivyo tuwasikizishe habari njema za neema hii wengine.

Neema hii ilimgharimu Mungu avae mwili na kuja kama mwanadamu ili tuu kutufikishia neema hii, nasi tukijua haya basi tufanye bidii kuyatenda mapenzi yake kazi ile aliyoifanya naam zaidi sana sawa na maagizo yake.
Nafurahi kuona una shauku ya kuipokea neema hii na wewe uliyeipokea unaendelea kuiishi neema hiyo, naam hata ikajaza mitaa yetu, mikoa na vitongoji vyake kwa utukufu wa Mungu.

Kwako usiye na neema hii, nina habari njema kwako kwamba ipo neema tele kwa ajali yako ipokee leo na uanze maisha mapya ya ushindi katika neema yake. 
Amen.

Comments