NI HUDUMA NGUMU SANA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU SANA!

Na Mchungaji Peter Mitimingi

Haya ni maelezo ya Mchungaji Peter Mitimingi ambaye pia mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM) akikuomba wewe unayesoma ujumbe huu kuhusika na jambo hili hapa chini, Maelezo ya Mchungaji Mitimingi ni haya.

  Nilimtembelea mchangaji huyu na kanisa lake siku ya Jumapili na kushiriki ibada pamoja nao. Mchungaji alitokwa machozi kwa furaha na mshangao mkubwa sana kwamba anaweza kukumbukwa na kutembelewa.

Alinieleza kwamba walikuwa wanaabudia nje kwa miaka 3 mpaka alipoamua kulazimika kuuza kiwanja chake alichonunua kwajili ya kujengea nyumba yake ili waweze kununua fito na udongo na makuti kwajili ya kujengea nyumba ya Mungu.


Aliuza kwa bei ya kulaliwa Tsh 300,000 laki 3 tu na akasema zote ziliishia kujenga jingo hili haikubaki hata senti ya kununua upande wa kanga wa mkewe.


Sasa makuti yapo upande mmoja na tayari yamesha chakaa ikinyesha mvua yanavuja akaomba tumsaidie apate bati waweze kujenga na kuimarisha nyumba ya Bwana. 


Yanahitajika mabati 25 na kila bati ni Tsh 16,500 kwa bati 25 ni sawa na Tsh 412,000 

NAOMBA WEWE UNAEGUSWA NA KAZI YA MUNGU UTUSAIDIE IDADI YA BATI KADRI BWANA ANAKAZO KUWEZESHA!!

Kutoa ni moyo wala sio utajiri, wasiliana na Mchungaji Peter Mitimingi kwa ajili ya sadaka yako ya ujenzi  wa kanisa hili  kwa namba   0713 183939.



Hili ndio kanisa linalotakiwa kujengwa.


Mchungaji Mitimingi akiwa na Mchungaji mwenyeji(Mwenye tai) pamoja na waumini wengine wa kanisani hapo

Comments