NILAZIMA UTAPIKWE

  
NA PST DAVID MWANGI WA UFUFUO NA UZIMAMOSHI.


YONA:2:10 Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.
Hii ni habari ya mtumishi wa Mungu kwa jina Yona, na kama mnavyojua huyu jamaa alikuwa ametumwa na Mungu kwenda Ninawi kuihubiri habari jema,Lakini badala yake akaamua kutoroka na kwenda Tarishishi,

Alifanikiwa kuingia kwenya meli moja, na walipokuwa wana endelea na safari kukatokea dhoruba kubwa mno, wale watu waliokuwa kwenye meli wakalazimika kutupa mizigo yao kwenye bahari ili waone kama meli itatulia ,

Walipokuwa wanasumbuka wakagundua kuna mtu mmoja ambaye alikuwa amelala, na walipochunguza wakagundua shinda yote ilikuwa kwake, na uamuzi  wao ulikuwa ni kumtupa Yona kwenye bahari ili kuponya nafsi zao,
Walipo mtupa Yona kwenye bahari , kumbe Yehova alikuwa ame andaa Samaki, ili kumpeleka kwenye hatma yake,Ilikuwa ni shinda kwa sababu Yona alikaa kwenye tumbo la samaki ,kwa siku tatu.

Yona akiwa ndani ya samaki akamlilia Bwana, naye Bwana akasema na Yule samaki naye akamtapika Yona pwani,
Ndugu na dada zangu leo niko na habari njema kwako wewe ambaye umemezwa na shinda, wewe ambaye umemezwa na magonjwa wewe ambaye balaa, mikosi, na nuksi zime kumeza,

MUNGU anaenda kunena na hali hiyo unayo ipitia, Mungu anaenda kunena na mdeni wako, Mungu anaenda kunena na biashara yako anaenda kunena na huyo Boss wako ambaye anakutishia kukufuta kazi, na atakapo nena ni lazima wataskia sauti yake kwa Jina la Yesu

Ninajua kuna watu wengi ambao walitupwa na watu wao WENGINE WALITELEKEZWA NA WAUME ZAO, WENGINE NA WAKE ZAO KWA SABABU YA SHINDA , Lakini leo niko na ujumbe wako, na ndio huu ya kwamba ni LAZIMAUTAPIKWE KWA JINA LA YESU
Fikilia samaki ali itii sauti ya Bwana, pia na hiyo shinda yako ni lazima ita tii sauti ya Mwokozi,Lazaro hata kama alikuwa amemaliza siku nne kwa kaburi haikumzuilia kuisikia sauti ya Yesu                                                                                                                 
,Bibli inasema katika Yohana 11: 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje., 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.

Ndugu mpendwa na kuhakikishi kwamba hiyo jangwa unayoipitia hutafia huko, kama vile Yona alitoka kwenye tumbo ya samaki na vivyo hivyo na wewe utatoka kwa Jina la Yasu Kristo wa Nazarethi
Nakuhakikishia ya kwamba ni wakati wako wa kutokea, ni wakati wako wa kubarikiwa ni wakati wako wa uponyaji, POKEA KWA JINA LA YESU

Comments