NIMECHOKA KUVAA MAGUNIA.

AP Hosea akihubiri ibada ya ijumaa jioni 4 July 2014

Na AP Hosea Shaban

Zaburi 35:1-14

“Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.
 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie.
 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
 Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.
Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.
Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia.Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu…………….”

Somo hili linaonekana la ajabu, hasa kwa sababu ya kichwa cha somo chenyewe kwamba tunavaa magunia hali tunaonekana tumevaa nguo Lakini katika hali ya huzuni, kuteswa na ugumu tunaokutana nao umebeba hali ya mtu aliyevaa magunia, (aombolezaye, asiye na furaha, aliyetengwa, asiyeishi katika matarajio yake na mwenye huzuni, aliyetengwa hata na marafiki zake n.k)

Lakini leo kuna habari njema kwa yeyote alionewa, aliyeishi maisha ya kupigana na kuishia kulia na umekosa furaha juu ya maisha yako “KWAMBA BWANA YUPO LEO ILI AKUPIGANIE ATETE NAO WANAOTETA NAWE NA KUKUPA UHURU WAKO”. Amesema Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Ni saa yako ya kulichoka tatizo lako, ukatae kuendelea kuishi na ugumu huo ulioupitia kwa mda mrefu, useme sasa basi kuvaa magunia haya ya (kukosa mtoto, kuugua kila mara na mwili wako kuwa nyumba ya magonjwa kwa kuzuruumia afya, kusimangwa, kuchekwa, kudharauliwa, kufedheheka, kuaibishwa na kuishi kwa machozi siku zote) na iwe zamu yao leo walionitega, wajinase wenyewe kwenye mitego yao, wanaopenda kuona nikilia walio wenyewe, Tunafanya vita dhidi yao, Bwana atete nao, wapigwe kabisa, waaibishwe, wafedheeshwe, njia zao ziwe giza na utelezi, malaika wa bwana akiwafuatia nyuma, wawe kama maakapi hata wakomeshwe kabisa.

Yavue magunia ya dhiki, kuonewa, kuaibishwa, kushindwa na uvikwe vazi la furaha
Mambo haya na yatendeke kwako na upokee ukombozi kamili katika jina la Yesu Kristo Ameni.

Comments