NITAWAPIGAPIGA WASIWEZE KUSIMAMA

Na.AP Hosea Shabban

Zaburi 18:36-38.

“Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.
Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe.
Nitawapiga-piga wasiweze kusimama, Wataanguka chini ya miguu yangu.”

Maishani mwetu kuna maadui wengi ambao wametesa maisha yetu kwa sababu ya kukosa maaarifa na kutosimama katika nafasi zetu.
Daudi alijitambua yeye ni nani na kwamba Mungu amemfanyizia nafasi hatua zake akasema nitawaafuatia adui zangu na watesi wangu na kuwapata, akasema wala hatua zangu hazitateteleka na kwamba hatarudi nyuma hata wakomeshwe, akasema nitawapiga-piga wasiweze kusimama tena, wataanguka chini ya miguu yangu.
Ukweli ni kwamba katika dunia hii na mbinguni hakuna jina litishalo na kuogopesha, iwe magonjwa, wachawi, umaskini, mapepo, majini na chochote kile kilichopo hapa duniani hakiwezi kutushinda kwa kuwa aliye ndani yetu ni MKUU kuliko vyote na kwa sababu hiyo mimi na wewe tuamue na kufanya vita dhidi yao;
HATUTETELEKI, TUNAZO NGUVU KATIKA KRISTO, ZAIDI AMETUPA MAMLAKA, TUTAWAFUATILIA, TUTAWAPATA, TUTAWAPONDA WAO NA NGUVU ZAO, TUBOMOA MADHABAHU ZAO, TUTAWAHARIBU NA KUWAPIGAPIGA KABISA, HATUTARUDI NYUMA, HATA WASIWEZE KUSIMAMA TENA, NAO WATAANGUKA CHINI YA MIGUU YETU!
Tunalituma NENO leo kwa maadui zako nalo litawafuata kama mshale ujuao adui zako, utapita katikati ya watu, milima, na mahali pote mpaka umpate adui yako na kumpata hata umpige na kumshinda kabisa. Mshale huu(HAUTAMKOSA) hata umpate, awe jini, mchawi, mganga mchawi, msoma nyota, mwenye kupindisha kesho yako, mwenye kutesa maisha yako na ubakie ukichanua.
Nakutakia Baraka ukiendelea kuyaishi mazuri yote aliyoyakusudia Bwana Kwako. AMENI.

Comments