NURU YA UZIMA. *Sehemu ya mwisho*

 Na Kabalama Masatu
Bwana Yesu asifiwe....

"Basi Yesu akawaambia tena akasema,Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,bali atakuwa na nuru ya uzima".Yohana 8:12.

ALELLUYAAAAAA......!
Ili kuipata nuru hii inakulazimu uifuate.
Kumbuka gharama za mianga mingine ni fedha ndipo upate huo mwanga.Lakini gharama ya Kristo ni kumkabidhi moyo wako na ndiyo maana anasema wazi bila kuficha ya kwamba "yeye anifuataye".
Huwezi kutaka kupata nuru ya uzima halafu wakati huo hutaki kufuata yule atoaye hiyo nuru.
Huwezi kutaka kutaka kuwa na nuru ya uzima katika maisha yako wakati huo wewe hutaki kuambatana na hiyo nuru.
Alelluyaaaaaa..........
Ninaposoma haya maandiko "Basi Yesu akawaambia tena akasema,Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,bali atakuwa na nuru ya uzima"*Yohana8:12; Napata hamu kubwa sana na wewe utambue siri kubwa sana iliyomo ndani ya Kristo.
Hebu mtoto wa Mungu fikiria kwamba Yesu Kristo ndiyo awe nuru ya maisha yako yote;maana yake yeye pekee ndiye ayaongoze maisha yako;maana hawezi kabisa kukupoteza bali atahakikisha yakwamba anakufikisha mahali sahihi.
Hakuna mwingine wa kukufikisha mahali sahihi hata baada ya kuwa umekufa isipokuwa Yesu Kristo peke yake.
Na ndiyo maana nakwambia habari hizi zilizo njema kabisa ili nawe uipate nuru;na kama tayari umekwishaipata basi na imlike kwelikweli maishani mwako wala usiizime kwa sababu yoyote ile.
Ukiifuata hii nuru basi umepata mwanga wa kuleta amani moyoni mwako.
Ni mwanga wa kuleta furaha maishani mwako.
Ni mwanga wa kuleta upendo katika familia yako.
Ni mwanga wa kutetea haki yako.
*MWISHO*
Mawasiliano:
0753-305957
0789-628226;
0717-624035.

Comments