NURU YA UZIMA.

 Na Kabalama Masatu

Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu katika kristo Yesu.
Karibu tujifunze habari zake Mungu kupitia jina la mwana wake,jina lenye nguvu kuliko majina yote,jina lenye kuokoa na kuponya,nalo ni jina la Yesu Kristo.
Somo la leo linaitwa NURU YA UZIMA.
#NURU-ni mwanga ambao unaweza kumwezesha mtu kuona mahali fulani wakati wa giza.
Hapa duniani kuna mianga ya aina nyingi sana ambayo watu wengi wanaiendea/wanaitumia.
Wakati wa giza watu wengi wanatumia vyanzo vya mianga walivyonavyo;wengine wanatumia tochi ya kawaida,wengine wanatumia tochi za simu,wangine wanatumia taa za kandili(chemli),wengine umeme,solar n.k.
Vyanzo vyote hivyo hutupatia mwanga ambao unatusaidia sana na hata tunakuwa na ujasiri wa kufanya jambo au shughuli yoyote hata kama ni wakati wa usiku maana tayari tuna mwanga.
Lakini pamoja na mambo yote hayo bado iko nuru moja ambayo ukishaipata hakuna kuwaza tena kwamba mbona giza limeingia,na kuanza kusumbuka kutafuta chanzo cha mwanga.
Nuru hii ni Yesu Kristo.
#Yohana8:12 imeandikwa:-
"Basi Yesu akawaambia tena akasema,Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,bali atakuwa na nuru ya uzima".
Umeona maandiko haya?
Maandiko yanasema wazi kwamba "mimi (Yesu) ndimi nuru ya ulimwengu".
Kumbe ipo nuru moja katika ilimwengu huu;nayo ni Yesu Kristo.
Hebu jiulize wewe katika maisha yako unatumia nuru ya namna gani?
Nataka uwaze juu ya nuru hii,#NURU YA UZIMA.
Kumbe siyo kweli kwamba unapompokea Yesu,umepokea hasara.#HAPANA!
Ila umepokea nuru ya kukumlikia katika ulimwengu huu na kukuonyesha njia yako ya kupita ili ufike mbinguni.
Ukimpokea Kristo umepokea nuru ya kukuongoza na kufika mbinguni ukiwa salama.
Ukimpokea Kristo umepokea nuru katika maisha yako,umepata nuru katika mipango yako,umepata nuru katika uhusiano (uchumba) wako, umepata nuru katika ndoa yako,umepata nuru katika masomo yako,umepata nuru katika biashara yako.


 
ALELLUYAAAAA....
#Yohana8:12:-
"Basi Yesu akawaambia tena akasema,Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,bali atakuwa na nuru ya uzima".

Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu.

Kumbe hiki ndicho kitu ambacho Bwana anataka tukijue;ya kwamba "yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,bali atakuwa na nuru ya uzima.
Kumbuka katika sehemu ya kwanza nilianza kuzungumza juu ya vyanzo mbalimbali vya nuru(mwanga).Hivyo basi inakupasa utambue kwamba hii mianga mingine ni sharti kiwepo chanzo fulani ndipo upate huo mwanga.
Ikitokea unatumia mwanga wa umeme basi uwe na uhakika ya kwamba mda wote Tanesco hawakati umeme,ikitokea wamekata umeme,basi na wewe hauna mwanga.
Kama unatumia tochi ya kawaida basi itakulazimu mda wote betri za tochi ziwe na nguvu.
Kama unatumia tochi ya simu uwe na uhakika kwamba betri ya simu yako ina chaji ili isije ikazimika.
Na hata kama ni taa ya kandili(chemli) basi lazima mafuta yawe kwenye taa.
Sasa hiki ndicho Yesu anataka tukijue ya kwamba ili upate nuru hii ya uzima ni lazima kwanza ufanye maamuzi magumu na mazito ya kuifuata nuru hii.
Sasa watu wengi wametamani sana kuipata nuru hii lakini wameshindwa kufanya maamuzi mazito.
Ndugu yangu huwezi kutaka kuingiza umeme ndani mwako wakati huo huataki kulipa gharama za kuwasababisha Tanesco wakuunganishie umeme;Haiwezekani;Nasema #HAIWEZEKANI!!!!!
Kwa hiyo jambo zuri ni kufanya uamuzi wa kumfuata kristo.

Ipo faida ya kumfuata Kristo:-
(i) Hautakwenda gizani;yaani siyo kwamba utapotea njia.Yeye anahakikisha unafika mahali salama.
(ii)Unapata nuru ya uzima;Yaani mauti iko mbali na wewe.
(iii)Unakuwa wokovu na kuwa nuru ya mataifa*Isaya49:6.
(iv)Nguvu za giza hazitakushinda tena*Yohana1:5.
Mimi nalipenda sana jambo hili la kumfuata Yesu ili anipe nuru ya uzima;wewe je?


ITAENDELEA.......
Mawasiliano ni:
0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments