OMBA KWA AJILI YA ISRAELI:Ndege zasitisha safari kuingia Israeli

Ndege zasitisha safari kuingia Israili.
Marekani imesitisha safari za ndege kuelekea kwenye uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion ulioko Israili.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kombora la wanamgambo wa Hamas kuanguka takriban kilomita moja u nusu kutoka kwenye uwanja huo.
Halmashauri inayosimamia usafiri wa ndege wa Marekani (FAA) imetoa amri hiyo dhidi ya mashirika matatu ya ndege yenye kuhudumu huko Israeli yaani Delta, United na US Airways dhidi ya kutua wala kuelekea Israeli kwa saa 24 zijazo ilikuipa (FAA) fursa ya kutathmini usalama wa abiria na wahudumu wa ndege hizo haswa wakati ambapo Israeli inakabiliana na Wapalestina huko Gaza.

Punde baada ya onyo hilo la (FAA) Mashirika kadha ya ndege ya bara uropa pia yalichukua hatua sawa na hiyo.
Mashirika hayo Lufthansa, KLM, na Air France pia yamesitisha safari kuelekea Tel Aviv.

Ndege zasitisha safari kuingia Israeli kufuatia tishio la usalama
Hata hivyo wizara ya Uchukuzi wa Israeli umekanusha tahadhari hiyo ikisema kuwa uwanja huo ni salama na kuwa hatua hiyo ya mashirika ya ndege ya Marekani imewapa mahasidi wao sababu kusheherekea.

Lufthansa - ambayo ni muungano wa mashirika ya ndege ya Uswissi, Ujerumani na shirika la ndege la Austria imetangaza kusitisha safari kuelekea Israeli kwa siku mbili.

Mashirika ya ndege ya KLM na Air France yameahirisha safari zilizokuwa zimeratibiwa kuanza jumanne.
Delta ambayo ilikuwa imeratibu safari ya ndege kutua Tel Aviv ililazimika kutua Ufaransa baada ya polisi nchini Israeli kudhibitisha kuwa kombora hilo lilitua kilomita moja nukta 6 kutoka kwenye uwanja huo wa Ben Gurion.

Shirika la ndege la Uingereza limesema kupitia kwa mtandao wa Twitter kuwa safari zake za ndege zitaendelea kama zilivyopangwa .
Kusitishwa kwa safari hizo za ndege zinawadia wakati Israeli ikiendelea na vita dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

 kwa mashirika ya ndege ni taharuki ya usalama wa ndege za abiria zinazopitia katika anga za mataifa yaliyo na vita haswa baada ya tukio la hivi punde ambapo ndege ya Malaysia MH17 kudenguliwa mashariki mwa Ukraine.

OMBA KWA AJILI YA ISRAEL.

Comments