ONDOA JIWE,ILI BWANA ATENDE.

Picha
Na Mtumishi Gasper Madumla
" Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? " Yohana 11:38-40

Bwana Yesu asifiwe sana...
Haleluya....

Ninayo furaha siku ya leo kukwambia pasword yako ya kufanikiwa kiroho na kimwili pia. Shida yako ni ugunduzi wa siri ya KUONDOA JIWE ILI BWANA ATENDE MAISHANI MWAKO. Jiwe lilopo kwako ndilo linakupelekea kusota kwingi.
Andiko hilo hapo juu;tunamuona Bwana Yesu akifika kaburini mahali alipolazwa Lazaro. Bwana Yesu hali akiugua nafsini mwake,anawaambia akina Martha jambo kubwa sana juu ya muujiza wa ndugu yao Lazaro. Jambo lile lile alilowaambia akina Martha ndilo analokuambia wewe siku ya leo,Bwana Yesu anakuambia ONDOA JIWE,ILI ATENDE.
Jiwe lillopo kwa Lazaro lilikuwa ni mithili ya ufupi wa Imani yao waliyokuwa nayo.Au lilikuwa mithili ya kwazo lizuialo muujiza wa Bwana.
Bwana Yesu angeliweza kumfufua Lazaro akiwa bado ndani ya lile jiwe,ila bado ingelikuwa hakuna utimilifu wa muujiza huo. Hivyo alihitaji waondoe kwanza jiwe ili afanye kazi yake. Hata siku ya leo Bwana Mungu anafanya kazi,achoki,alali,wala hasinzii,sasa,ili kazi yake ipate kudhihilika ndani yako,huna budi KUONDOA JIWE.
Tazama,
Bwana Yesu alijua siri ya kudhihilisha utukufu wake,ndio maana kwanza aliwahitaji akina Martha waondoe jiwe.
Hakuna muujiza wowote unaotokea mahali penye jiwe,( chukua hilo kwa faida yako siku ya leo) Maana hata ufufuko wa Bwana Yesu,ulihitaji jiwe kuondolewa.
Maana imeandikwa;

" Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini" Yoh.20:1
Bwana Yesu asifiwe....
Ukitaka kuuona utukufu wa Bwana,ondoa jiwe
Ukitaka kuchomoka katika hiyo hali uliyonayo sasa,ondoa jiwe ili Bwana atende.
Maana yawezekana kwako;
Jiwe ni kutokumiani kwako,Au
Jiwe ni UCHUNGU ulio ndani yako,Au
Jiwe ni HASIRA iliyo ndani yako,Au
Jiwe ni KUSHINDWA KUACHILIA mambo yaliyoshika moyo wako. N.K

Haleluya..
Nasema,Haleluya...
Sema Amen.

Yupo mtu ambaye jiwe lake lilikuwa ni UCHUNGU uliokamata moyo wake.UCHUNGU uliotokana na kuumizwa na mtu wake wa karibu. Mtu huyu alikuwa ana muamini Bwana Yesu Kristo kwamba atatenda juu ya shida aliyokuwa nayo,lakini hakupokea muujiza wake kwa takribani muda mrefu, sababu JIWE LA UCHUNGU lilizuia huo muujiza.
Pale aliposhughulikia siri ya tatizo la kuondoa shina la uchungu ndani yake,alikuwa sawa sawa ameondoa jiwe ndani yake,na kuanzia hapo Bwana mzee wa siku akatenda. Akapokea mara moja muujiza wake.
Mimi sijui kwako mpendwa,ni jiwe gani lilozuia muujiza wako,maana kama kuomba yawezekana kabisa umeshaomba vya kutosha, lakini bado hukupata chochote,Sasa ni wakati wa kujichunguza kwa upya na kuondoa kila aina ya jiwe ndani ya moyo wako,ili Bwana atende.
Tazama Bwana Yesu akimwambia Martha;
" Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? " Yohana 11:40"

Ndivyo akuambiavyo hata wewe siku ya leo. Anakutaka kwanza uamini,ili ukauone utukufu wa Bwana. Ukiamini,atafanya.
Mambo yote magumu kwako,kwa Bwana ni mepesi kama nini.
Hata Musa aliwataka wana wa Israeli waamini,ili Bwana akawatendee mambo makubwa,tazama tunasoma;

" Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele." Kutoka 14:13
Nami nataka nikutangazie kwamba,ukiondoa jiwe lako,ukaamini,UTAUONA WOKOVU WA BWANA.
Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...
Nasema hivi;
Bwana Yesu asifiwe....
Kama unaamini sema AMEN.

Siku za leo,watu wengi wamezingilwa na JIWE LA ROHO YA UDINI.
Roho ya udini ni jiwe tosha la kuzuia muujiza wako. Wapo watu waliokamatwa na roho hii ya udini,wakijiita " sisi ni wa dini fulani,,.." Au " sisi ni wa dhehebu fulani"
Sikiliza nikuambie ndugu,kwamba YESU HANA DINI,WALA DHEHEBU BALI ANA WOKOVU TU,YEYE NI BWANA WA mabwana.

Kati ya vitu sivipendi duniani pindi nchi idumupo ni roho ya kunga'nga'nia dini,wakati MUNGU wetu hana dini. Ondoa hilo jiwe,njoo kwa Yesu,UOKOKE ili Bwana atende.
Ikiwa lipo jiwe la aina yoyote ile ndani ya maisha yako,lenye kuzuia kupokea mambo makubwa yatokayo kwa Baba wa mbinguni,nawe umelichukia jiwe hilo, basi usisite kunipigia simu yangu,ili tuombe pamoja kungo'a kila aina ya pando lisilotokana na BABA wa mbinguni,
Ikiwa unaamni hayo,basi unipigie simu,na kama huamini usinipigie,
Namba yangu ni hii;
0655-111149.

UBARIKIWE.

Comments