shetani NDIYO CHANZO CHA MABAYA YOTE YANAYOMKUTA MWANADAMU LEO.

 
-shetani ni muongo.
-shetani alisababisha kifo.
-shetani anatafuta wa kumsindikiza jehanamu.
Ndugu yangu jitahidi sana kuzitambua hila za shetani maishani mwako, maana shetani anaweza akaja na kaukweli kidogo ili akuteke kumbe kisha akuangamize.
-shetani anawadanganya baadhi ya watu kuua wazazi wao ili tu wawe matajiri kumbe ni mbinu yake ya kuangamiza wazazi na mhusika.
Tumpinge shetani naye atatukimbia(Yakobo 4:7)
shetani hafai.
Hapa chini kuna chanzo cha maovu duniani ambapo shetani kwa kutumia sura ya nyoka alimdanganya Eva na kupelekea kila aina ya mateso kwa mwanadamu.
ona jinsi ambavyo shetani alianza na ka ukweli kidogo ili kumteka Eva.
Karibu
Mwanzo 3:1-19 inasema ''Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA MUNGU. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema MUNGU, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani MUNGU amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
kwa maana MUNGU anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama MUNGU, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Kisha wakasikia sauti ya BWANA MUNGU, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA MUNGU asiwaone. BWANA MUNGU akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA MUNGU akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala. BWANA MUNGU akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa
maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.''

Ndugu zangu tunatakiwa tuwe watu wa rohoni sana ili kumshinda shetani.
watu wengi shetani amewaondolea nguvu ya maombi ili tu connection yao na MUNGU iondoke ili shetani awamiliki na kuwasababishia jehanamu ya moto.
Ndugu yangu kaza mwenda na YESU mwenye uzima wako wa milele.

Dhambi ililetwa na shetani na Imepelekea Kupungua Umri Wa Kuishi. MUNGU Alipanga Mwanadamu Aishi Milele Yaani Awe Na Mwanzo Tu Ila Mwisho Usiwepo Lakini Dhambi Ilipoingia Miaka Ikapungua, Kwa Upendo Wa MUNGU Adamu Akaishi Miaka 930, Nuhu 950 Lakini Cha Ajabu Wanadamu Hata Hiyo Ofa Wakaikataa Kwa Kuongeza Maovu Duniani, MUNGU Akapunguza Miaka, Ibrahimu Akaishia Miaka 175 Na Isaka 187, Hata Hii Ofa Ya Pili Wanadamu Hawakuitaka, MUNGU Akapunguza Miaka Ya Kuishi, Yusufu Akaishi Miaka 110 Na Daudi 120, Wanadamu Bana Hata Hii Ofa Mpya Hawakuitaka MUNGU Akapunguza Kidogo Ili Wabadilike Lakini Wapi, Yohana Akaishi Miaka 98 Na Moses Kulola Miaka 83. Hebu Ona Tofauti Ya Miaka Kwa Vizazi Hivi Enzi Za Watu Hawa Wa MUNGU. Ndugu Zangu Tuiambieni Dunia Iache Dhambi Maana Wastani Wa Sasa Wa Kuishi Ni Miaka 80 Na Kwa Neema Ya MUNGU Na Kwa Sababu Maalumu Vyombo Viteule Vya MUNGU Kama Moses Kulola Wanavuka Wastani. Sasa Muda Wa Kupunguza Umri Unakaribia Na Kwa Uovu Wa Sasa Kuna Uwezekano Wa Umri Kufikia Mwisho Miaka 18 Yaani Ukianza Tu Uovu........
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292 
                     mabula1986@gmail.com
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.
 

Comments