SIFA SABA ZA IBADA NJEMA.



BWANA YESU asifiwe watu wa MUNGU.
Ni jumapili njema ambapo wengi wanaenda makanisani kumwabudu MUNGU aliye hai.
Mimi nakutakia ibada njema sana na sifa za ibada njema ni hizi.

1. Ibada njema ni ile ambao waabudu wanamwabudu MUNGU katika Roho na Kweli(Yohana 4:24)

2. Ibada njema huanzia nyumbani.

3. Ibada njema ni ibada inayoambatana na sadaka na fungu la kumi kama kumshukuru MUNGU kwa alivyotupa na kuonyesha unyenyekevu kwake aliyetupa kipato.

4. Ibada njema ni ibada ambayo waamini wameitoa dhabihu miili yao ili kumpendeza MUNGU.

5. Ibada njema ni ili ambayo waamini wanamwabudu JEHOVAH (Zaburi 83:18)

6. Ibada njema ni ile ambayo waamini wake wamempokea BWANA YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yao.(Yohana 1:12-13, Matendo 4:12 na Yohana 14:6)
 
7. Ibada njema ni ile ambayo waamini wanaongozwa na Roho wa MUNGU (Wagalatia 5:20).

Ubarikiwe sana kwa kulijua hili na naamini kabisa wewe na mimi tutaenda kumwabudu MUNGU BABA katika Roho na kweli na ibada yetu itakuwa njema.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292.
Mabula1986@gmail.com.
UBARIKIWE SANA ULIYESOMA UJUMBE HUU.
Hapa nakupa nyimbo 2 video ambazo zinamtukuza MUNGU kutoka kwa Fanuel Sedekia na Upendo Nkone, ziibariki jumapili yako.






Nikiwa Zanzibar kihuduma.

Comments