SIFA ZA MWANAFUNZI WA YESU.

BWANA YESU asifiwe.
Na Lucy Marandu


Mwanafunzi wa YESU hana  tofauti na mwanafunzi wa Shule

MAANA YA NENO MWANAFUNZI NA LENGO LA UANAFUNZI NI; KUJIFUNZA ILI UFUZU.

Kama ambavyo mwanafunzi wa shule yoyote ni wajibu wake kuhakikisha ana;
1) DAFTARI
2) KALAMU
3) VITABU

Vivyo hivyo Mwanafunzi wa Yesu, ni wajibu wako kuhakikisha una
1) DAFTARI (DIARY)
2) KALAMU
3) KITABU (BIBLIA)

Kwa ajili ya kuandikia notes kwa manufaa ya kujifunza na kujikumbusha tena na tena juu ya kile alichojifunza!

Sasa mimi huwa nasikitishwa sana, kuwaona baadhi ya watu wanakwenda kanisani bila vitendea kazi! Sijui huwa wanawaza nini, maana ni ngumu sn kuyakumbuka yote uliyojifunza bila kuweka kumbukumbu!

IKUMBUKWE KWAMBA;

Sisi sote tulio wanafunzi wa Yesu, hakuna aliyefuzu bado,Wala hakuna mjuaji zaidi ya biblia, bali wote tupo katika mchakato wa kujifunza njia sahihi za kumpendeza Mungu.

Hivyo basi, imetupasa, kujinyenyekeza katika kujifunza kwa kuweka kumbukumbu za masomo tuliyojifunza ili hata tukikutana na kwazo lolote tuweze kuyarejea masomo yetu kama mwongozo! Na hapa hakuna mjuaji, mwalimu wala nani! Ni sisi sote!

Tuache tabia ya ubosi,ya kujifanya wajuaji! Kwamba haina haja ya kubeba biblia, daftari na kalamu! kwani tutaelewa tuu! Kumbuka shetani yuu pembeni yetu teyari kuyapeperusha yale tuliyoyasikia punde, lkn tukiwa tumeandika ni rahisi kujikumbusha tena na tena.

HUWEZI KUFAULU(KUSHINDA) USIPOTIA BIBII YA KUJIFUNZA

Biblia inazungumzia YEYE ASHINDAYE atayarithi haya....
Ufu 2:7, 2:11, 2:17, 2:26, 3:5, 3:12, 3:21, 21:7.

Ahaaa kumbe hapa duniani tunashindana?? Sasa kama tunashindana kweli tutaweza kufuzu ikiwa hatuna material ya kutosha katika kushindana?? Tunaona wanafunzi wa shule wanaenda katika maktaba flani flani kwa ajili ya kutafuta matirial jee sii zaidi sana sisi wanafunzi wa Yesu, tukaichimbua biblia kwa kupata maarifa zaidi ya kutuwezasha KUSHINDAA??

RAFIKI YANGU MPENDWA;
Acha U-staff wa kijinga, KWA YESU HAKUNA STAFF!

Na pia tuwakimbie hawa walimu wa Mishahara, wanaotuona tukiingia kanisani bila vitendea kazi, lkn hawaoni mzigo wa kutufundisha na kutuelewesha lile litupasalo kutenda! Wao hujisemea moyoni mwao shauri yao wenyewe, wafaulu kuingia mbinguni au wasifaulu shauri yao!


NB: Sisemi mchungaji afanye kazi ya kuwakagua laa hasha,NI PALE APATAPO UFUNUO! Lakini pia, wapo baadhi ya makanisa asili yao hawana mda wa kuandika notes kabisa! Wajirekebishe!

Mungu akubariki sana.

By Lucy Marandu.

Comments