TAWALA ULIMI WAKO

Na Nabii Samson Mboya kutoka Geita Piga simu 0756 809209ushauri na maombezi
Utangulizi:

Ukitaka Mema katika maisha yako basi anza wewe kufanya mema kwanza  usitake kuvuna katika shamba ambalo hujalipanda kitu, ukitaka Baraka anza kubariki wengine kwanza, ukitaka heshima  heshimu wengine, ukitaka kupendwa penda wengine ukitaka kuongelewa vizuri na wengine  ongelea wengine vizuri kwanza, kila jambo unalo litaka katika Maisha yako  funguo za kufungua au kufunga unazo wewe mwenyewe,

Maandiko Matakatifu yanaongelea nini juu ya funguo hizo,

Mathayo 16:19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa  pia  mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa  pia mbinguni."


Bila ya kupewa funguo yaani uwezo mpya katika kinywa chako huwezi kufunguwa au kufunga chochote katika hii Dunia ,

Unaweza ukawa huru lakini ,usiwe na uwezo wa kufunguwa au kufunga  chochote  ukisha zaliwa mara ya pili fahamu kuwa katika ulimi wako unawekwa uwezo wa kufunga na kufunguwa chochote kile unachokitaka hata uzima na mauti,

Mithali 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake

Ø  Hatari ya kutochunga Ulimi

Ø  Usipo chunga ulimi wako Unaweza ukashiba mauti/ukafa ki-mwili na ki-roho

Ø  Usipo chunga ulimi wako unaweza ukauwa wengine

Ø  Usipochunga ulimi wako unaweza ukawanyima wengine Mbingu

Ø  Usipochunga ulimi wako unaweza ukauwa huduma za wengine ki-mwili na kiroho

Ø  Usipichunga ulimi wako unaweza ukanajisi maisha yako bila wewe kujuwa

Ø  Usipochunga ulimi unaweza ukayakoroga maisha yako

Ø  Usipochunga Ulimi wako unaweza ukaharibu kipaji/zawadi yako

Ø  Usipochunga ulimi wako unaweza ukajilaani bila kujuwa

Ø  Usipochunga ulimi wako unaweza kujifunga wewe mwenyewe bila kujuwa,

Chunguza nini umejitamkia katika maisha yako au katika maisha ya mwezako kile unapanda tarajia kuvuna, hicho hicho, kumbuka laana na baraka zinapitia katika kinywa, chunga ulimi wako,

Yakobo 3:10  Maneno ya laana na ya kusifia  hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.


Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwapia mbinguni."
Mathayo 16 : 19

Usipokuwa makini na Ulimi wako huwezi kupewa uwezo wa kufungua au kufunga kwakuwa utafunga visivyo fungwa na utafunguwa visivyofunguliwa  na hii ni moja wapo ya sababu ya wewe wengine kila siku hawaoni mabadiliko kwakuwa hawatumii ulimi sahihi

Usipokuwa na Neno la Mungu ndani moyo wako na wewe ukataka kunena  yaliyoakilini mwako  unaweza ukajitengenezea aibu, ambayo kuifuta itakugarimu sana,au isiondoke kabisa, si lazima kila unachokiona nilazima  ukiongelee au si kila unachokisikia lazima ukiongelee, ukimya nao ni majibu pia

Tito 2:7  katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,
8 na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.

Kila unalofanya uwe mfano wa kuigwa kwa wengine  ukiongea Neno kila mmoja alitamani kulitumia ,katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, usiwe mwepesi wa kuongea uwe mwepesi wakusikia lakini mzito wa kuongea, siyo unakuwa mwepesi hadi unajikwaa unamkosea Mungu

Chunga ulimi wako  juu ya kile unachotakakukisema kwakuwa fahamu unapanda sasa katika kupanda kaguwa unapanda nini, maana subiri kuvuna baada ya kupanda,

  Mathayo 12:22H apo watu wakamletea Yesu kipofu mmoja ambaye alikuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Yesu akamponya hata, akaweza kusemana kuona.


ulimi unatumika sana na Mungu  kufanya mapenzi ya Mungu na Mapepo yanataka sana  kutumia kinywa hicho hicho  kuwa na Maneno mengi sana yasiyo ya ki-Mungu ni Roho ya mapepo inakuwa inamtumikisha mtu kuongea Dawa ni kumuombea sala ya toba,

Markop 9:17 Hapo mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, "Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.

Ukiona huwezi kushuhudia hata neno mmoja kwamba umeokoka au Mungu amekutendea nini, fahamu wewe ni utakuwa na roho inayokuzuwia kunena, kwakuwa utamwaibisha shetani na yeye hataki aibuna hii ni sababu mmoja wapo Mtu anapozaliwa maya ya pili awali anakuwa moto sana baada na kitambo anajikuta kimywa kabisa sababu nini? Amevamiwa akabigwa na ububu,

Luka 1:20 Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayoniliyokuambia yatakapotimia."


Upo wakati Mungu anaweza kukunyamazisha kwa sababu maalumu anazozijuwa yeye  unaweza ukaenda maeneoflani Mungu akakuzuwia kuongea kabisa hata ukijilazimisha unashindwa, kama anavyoweza kukulazimisha useme Neno mahalifulani ulipo,

 

1 Wakoritho 14:9Hali kadhalika na ninyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.


Kunawatu kutwa nzima nikupoteza tu chunga ulimi wako usijeukapotesa hewani maneno,


Yakobo 1:26 Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.


Yakobo 3:5 Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. ic Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.


Yakobo 3;6 Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote.Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.


Lakini hakuna mtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.
Yakobo 3 : 8


Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Yakobo 3 : 9

 

Zaburi ya 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

Kile kilichomjaa mtu moyoni ndicho anakinena  hivyo kumfahamu huyu nimtu wa namna gani ni Rahisi sana kupitia ulimi anajitambulisha ndani ya mtu kukiwa na uzima atanena uzima kukiwa na mauti atanena mauti,

Maombi

Mathayo 3:8 Basi zaeni matunda yapasayo toba;


Matendo ya mitume 11:18 Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.

Anza kumtamkia mema yule uliyekuwa umemsababisia matatizo kwa ulimi wako wengine uliwakwaza ,ukawaua ki-Roho na kimwili omba sasa,

Comments