TENA NASEMA FURAHINI


Na Ap HOSEA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA (MOSHI)
 Wafilipi->4:4-7 “ Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu” 

*Watu wengi leo duniani hawana amani wala Furaha kwa sababu ya mambo fulani Fulani yaliyojitokeza maishani mwao yamkini wewe unayesoma maneno haya ya uzima ni mmojawapo kati ya hao walio koseshwa furaha,Ahimidiwe Bwana wa majeshi kwa maana yeye ndiye Furaha ya maisha yetu! 



SABABU CHACHE KWA NINI TUFURAHI KATIKA BWANA 

1/Tunafurahi katika Bwana tukijua katika Bwana Imo furaha na amani ya kudumu. 

2/Tunafurahi katika Bwana kwa maana ukimpokea Bwana Yesu nguvu za giza hazina uwezo juu ya maisha yako tena! 

3/Tunafurahi katika Bwana kwa maana kuna mataifa wanategemea kuona vitu kutoka kwetu,Ambavyo vitabadilisha mtazamo wa maisha yao! 


Majeshi ya Bwana yakishagilia pindi yalipotambua Furaha ya kweli ni Yesu pekee.

*Maandiko yanasema Upole wenu na ujulikane na watu wote kwa maana Bwana yu karibu ni lazima upole wetu ujulikane na watu wote ili watu wapate kujifunza kutoka kwetu . 

*Tatizo la watu wengi wanapoumizwa na kukoseshwa amani na furaha,huwa wanaangaika na kutafuta msaada wa kutatua matatizo yao kwa wanadamu,Bali leo Eeh mtu wa Mungu nakusihi kwa jina la YESU KRISTO chukuwa hatua ya kumgeukia Mungu na kuamini ya kuwa yeye ndiye njia pekee ya kutatua matatizo yaliyokukosesha furaha maishani mwako. 

*Tunaona hata mtumishi wa Mungu Daudi katika shida yake hakuwaita wanadamu,Bali alitambuwa msaada wake unapatikana kwa Bwana YESU pekee,Naye akageuza mtazamo wake kutoka kwa wanadamu na akachukua hatua ya kumuamini Mungu pekee kwa Imani yake yote,Ni maombi yangu mbele za uso wa Mungu jioni ya leo uchukuwe hatua ya kuondoa tegemeo lako kwa wanadamu na kuliamishia kwa Mungu kwa maana Imeandikwa “Amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu na moyoni mwake amemuacha Bwana. 

*Yakupasa kufahamu kuwa unapoingia kwenye matatizo au shida mbali mbali zitakazoweza kuitowesha furaha ya Mungu maishani mwako ni lazima ujifunze akilini mwako wa kumuendea ni nani? Na ni jambo jema tena lafaa kama nini! kupeleka haja za mioyo yetu kwa Bwana Yesu! Pia ni lazima ufahamu ya kuwa umembeba nani! Ndani ya moyo wako kwa sababu kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipita katika vipindi vigumu maishani mwao kwa sababu hawajajua waliye naye ni Mkuu kuliko mkuu wa Ulimwengu huu! 
Makamanda wa Bwana Yesu wakimsihi Bwana Yesu kuwa furaha pekee ya maisha yao




Comments