TUMAINI KATIKA DHIKI

Na Pastor David Mwangwi; UFUFUO NA UZIMA KILIMANJARO
 
Mpendwa dunia tunayo ishi imejaa dhiki na uovu, mpaka unapoangalia mahali unapoweza kujificha unakosa, Lakini na ashukuliwe Mungu wa uzima ambaye anatuahidi tumaini hata katika mambo hayo.
Watu wengi duniani wanakaa kama watu ambao hawna tumaini , kwa sababu hawajui wakimbilie wapi,, Lakini Usiku wa leo niko na habari njama kwa ajili yako kwa sababu Yesu Kristo mwana wa Mungu yu hai na analo jawabu la maisha yako



Katika maandiko matakatifu ya Mungu neno lina sema  .
AYUBU 14:7 Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.
 8 Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo;
 9 Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche

Mungu ana nena na wewe usiku wa leo na anasema kuna tumaini kwa wale wote ambao wanaona nikama dunia imefika mwisho.
Wana wa Israeli waliteseka sana mikononi mwa wa Misri, lakini siku moja Mungu alishuka na kuwapa tumaini kwamba anajiandaa kuwatoa huko kwenye mateso, Na vivyo hivyo SIKU ya leo Bwana ameshuka leo ili akuokoe.

Ndugu mpendwa niko na habari njema kwako siku ya leo, kwa maana bwana amenituma nikwambie ya kwamba uwe na subira, kwa maana yuko njiani akija kukuletea Baraka zako
Kuna uwezekano uli mwendea daktari na alipo kupima akakwambia uko na H.I.V au CANCER , na zaidi akakwambia haya magonjwa hayana tiba, LAKINI  MIMI niko na habari njema kwako na hiyo habari ndio hii ya kwamba         ISAIAH 53: 5 Inasema,  Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
   
Kuna uwezekano siku ya leo, umefika mwisho katika maisha, unapoangalia mbele na nyuma hauoni tumaini lolote, lakini nataka nikutie moyo ya kwamba kesho mema yapo,kwa maana imeandikwa katika , Isaya 3:10 Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao
 
Nina nena na wewe uliye poteza tumaini, wewe ambaye umeitafuta kazi kwa miaka mingi ukakosa, wewe ambaye madaktari walisema huwezi kuzaa,wewe  ambaye ndugu na jamaa zako walikufukuza nyumbani  sababu ya shinda, wewe ambaye una matatizo ya ndoa, Mungu anakuja kukuondolea msiba na matatizo ya maisha yako.

Ndugu zangu msife moyo, lakini muwe na moyo mkuu, mkijua mateso mnayopitia ni ya muda tu, Kuna utukufu ambao unakungonjea, Endelea kuliitia Jina la Bwana wa majeshi,
                              BWANA AWABARIKI SANA
 
.

Comments