UCHUMBA MTAMU LAKINI NDOA CHUNGU.




Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke unaokubalika kiutamaduni na kidini ambao unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kijinsia na kutosheleza majukumu mengine ya kijamii. Katika ndoa kuna uhalali wa watoto.


Pamoja na tafasiri hiyo ya ndoa, watu wengi siku hizi wamekuwa wakiishi maisha ya ndoa kama fasheni hali ambayo imekuwa ikishusha hadhi ya ndoa. Si jambo la ajabu kusikia ndoa iliyofungwa wiki moja iliyopita imevunjika baada ya wanandani hao kutwangana makonde.


Katika ndoa kuna matabaka mawili. Tabaka la kwanza ni kwa wanandoa kufurahia ndoa yao na tabaka la pili ni la wanandoa kuijutia ndoa yao. Hakika ndoa inaraha sana na nitendo la heshima mbele za MUNGU.
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini siku ya harusi wanandoa wote huwa na furaha? Na je, furaha hiyo baadaye hupotelea wapi? Hakuna mwanandoa yeyote ambaye huwaza kama siku moja yeye na mwenzi wake wanaweza kukorofishana na kutukanana matuzi mazito ambayo hugeuka kuwa sumu ndani ya ndoa yao.


Siku ya harusi kila mmoja huisubiri kwa shauku kubwa na kuona siku kama haziendi ili wanandoa hao wawe pamoja katika jahazi la ndoa ya maisha. Lakini mambo hubadirika kwa baadhi ya wanandoa pindi wanapoanza maisha ya pamoja. Kabla sijaendelea naomba kukuuliza wewe uliyendani ya ndoa, je ulishawahi kujiuliza ni kwanini furaha mliyokuwa nayo wakati hamjaoana leo hii haipo hivyo? Kumbuka mara nyingi upendo unaotolewa wakati wa uchumba huwa una mbinu nyingi za kusomana tabia na kila mmoja hupenda kuficha tabia yake mbaya aliyonayo. Ni suala gumu kidogo kwa wanandoa ambao kila mmoja amekulia katika malezi tofauti kukaa na kujenga tabia moja. Wakati watu wanapokuwa katika hatua ya uchumba hushindwa kusomana vizuri tabia zao kutokana na umbali walionao. Kwa sababu kila mmoja anakuwa kwao ama kwake hali ambayo hutoa muda mwingi wa kumkumbuka mpendwa wake.

Kipindi hicho wachumba hao hutumiana jumbe fufi kupitia mitandao kama simu na email ili kila mmoja kuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda mwanandani wake mtarajiwa. Wahusika hao hujitahidi kutumika maneno mazuri na yenye kuvutia hisia pande zote mbili. Maneno hayo huongeza shauku kwa walengwa hao kuwa na shauku ya kuwa pamoja wakidhani kuwa siku zote mambo yatakuwa hivyo.


Kwa kipindi hicho wachumba hao huwa wanaelewana kwa kila jambo wanalopenda lifanyike. Utamu wa uchumba huo kama nilivyosema hapo awali hunogeshwa na umbali uliopo kati ya wahusika hao. Wakati mwingi mmoja wapo anapotakiwa na mwenzake wakutane sehumu wanayoona inafaa kwa ajili ya mazungumzo yao ya faragha hulazimika kuwadanganya wazazi wao ama ndugu zao wanaoishi nao kwamba wanaenda kwa jamaa zao na atachelewa kurudi.


Na pindi mazungumzo yao yanapoanza huku muda ukizidi kwenda wachumba hao hutamani muda urudi nyuma ili waendelee kuongea na kupeana habari za hapa na pale kuhusu maisha yao ya badae. Sasa shauku hiyo ya kuwa pamoja hupotelea wapi baada ya kuoana ambapo huwa kuna muda mrefu wa kuwa pamoja tofauti na kipindi kile walipokuwa wanaona muda unaenda na mazungumzo yao bado yanaendelea?


Nadhani utaungana na mimi kwamba kwa baadhi ya wanandoa mambo hayo hupotea pindi wanapoingia ndani ya ndoa kutokana na muda mwingi kuwa pamoja. Utakuta wanaongea masuala yao mpaka yanaisha. Na kisha wanalala. Siku zote mwanadamu hakosi kuwa na madhaifu maishani mwake. Kipindi hicho wanandoa hujikuta wapo katika wakati mugumu pindi mmoja wapo anapofanya kosa hata si kwa makusudi. Inawezekana akawa ni mama akawa mkorofi ama baba ama wote kwa pamoja. Na hiyo hutokea kila mmoja kujiona anahaki ya kufanya atakavyo na hayupo tayari kukosolewa.


Ni imani yangu kuwa kila mwanandoa siku ya kufunga ndoa huwa kunaviapo ambavyo hutamkwa na wahusika wote. Kwamba watakuwa tayari kuishi katika maisha ya raha na shida, iwe magonjwa nk. Lakini mambo huwa sivyo pindi safari ya maisha ya ndoa yanapo anza.
MUNGU akubarikikwa tafakari hii ya ndoa.


By  Melchiory Kasmiry

Comments