
Watu wengi hawapendi mahubiri wala habari za semina za neno la MUNGU lakini mimi naomba waelewe hivi.
Kuna Siku Mchungaji Mkuu Atawabagua Kondoo Na Mbuzi, Kondoo Wataenda Uzimani Na Mbuzi Wataenda Motoni, Mchungaji Mkuu Ni BWANA YESU, Kondoo Ni Waliompokea Yeye Kuwa BWANA Na MWOKOZI Wao Na Mbuzi ni Waliomkataa Yeye. Ndugu Yangu Hakuna Uwezekano Wa Kulala Ukiwa Mbuzi Ili Uamke Ukiwa Kondoo Bali Ukiwa Hai Tena Ukiwa Na Fahamu Zako Zote Unaweza Kwa Dk 1 Kubadilika Kutoka Mbuzi Na Kuwa Kondoo. Baba Na Mama, Kaka Na Dada Ni Heri Kuwa Kondoo Na Sio Mbuzi.(Mathayo 25 : 31 - 46)
Ndugu Yangu Leo Nimekuja Na Habari Njema, Kama Ukimkiri YESU Kwa Kinywa Chako Ya Kuwa Ni BWANA Na Ukaamini Moyoni Mwako, Utaokoka - Warumi 10:9.
Ulipozaliwa Kwa Mara Ya Kwanza Ulifanyika Mtoto Wa Wazazi Wako Wa Kimwili Lakini kama Utazaliwa Mara Ya Pili Utafanyika Mtoto Wa BABA Yako Wa Mbinguni( Yohana 1:12, Yohana 3:1-14)
-Ndugu Yangu Mwombe MUNGU Akupe Moyo Wa Kulisikiliza Neno Lake Na Kulitii, Ili Upate Kuwasaidia Na Wengine.
- Ndugu Yangu Nakuomba Umwombe BWANA MUNGU Ili Ayabadilishe Maisha Yako, Yawe Kama Yeye Atakavyo Na Sio Wewe Utakavyo.
- Ndugu Yangu Muombe MUNGU Akulinde Na Hila Za shetani, Patana Na Uliowakosea Wote Na Fanya Jitihada Za Kuwa Na Biblia Yako Mwenyewe.
-Ukipenda Ua Penda La Boga Lake, Ukipenda Kuponywa Mpende Na Mponyaji, Ukipenda Uzima Mpende Na YESU Anayewapa Watu Uzima Wa Milele.
Tambua kwamba Ajali Mbaya Zaidi Ni Kufanyika Mtoto Wa MUNGU Harafu Ukashindwa Kukua Kiroho.
Parapanda Italia, Wateule Watakua Wamenyakuliwa Kwenda Kumlaki BWANA YESU Mawinguni Chini Watabaki Walevi, Wazinzi, Waasherati, Majambazi, Waongo, Waabudu Sanamu, Wachawi, Waganga Wa Kienyeji, Mashoga, Freemason, Matapeli, Wanaomkataa YESU Leo Na Watenda Dhambi Wote. Ndugu Yangu Hata Kama Umefanya Dhambi Zote Nilizotaja Hapo Juu Ukimpokea BWANA YESU Leo Atakusamehe Na Utajumuika Na Wateule Kama Ukidumu Katika Utakatifu. YESU Anakuhitaji Sana Kuliko Wanavyokuhitaji Wanadamu Wote, Amua Tu Leo Kumpokea Ili Awe BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako, Soma Yohana 14 Yote, Matendo 4:12 Na Yohana 3:16.
Ndugu Yangu Ni Hatari Sana Kama Usipompokea BWANA YESU Leo.
Baba Na Mama Acheni Dhambi, Vijana Wa Kiume Na Wa Kike Acheni Dhambi Maana Dhambi Ni Mbaya, Baada Ya Kifo Ni Hukumu, Na Kadri Tunavyoiona Siku Mpya Ndivyo Na Saa Ya Kufa Inasogea.
Na wewe mtumishi wa MUNGU Tambua Kwamba Neno La MUNGU Linatambua Mawazo Ya Kila Mtu, Wewe Litamke Tu Litafanya Kazi Yake Kwa Mlengwa Hata Kama Uliowapelekea Neno Hilo Wamekubeza, Neno Litaanza Kufanya Kazi Yake Hata Baadae.
Comments