USIDHARAU NDOTO ULIYI IOTA

 
                    
  NA  SNP :MWANGASA, Ufufuo na Uzima Moshi Kilimanjaro.
                        
Kwenye Biblia kuna watu wengi waliota ndoto na tukiziangalia karibu zote zina uhusiano na Mungu.

Kwa mfano ndoto ya kwanza kabisa kwenye  Biblia inapatikana kwenye kitabu cha mwanzo 20:1_7,
Hapa tunamuona mwotaji Abimaleki Mfalme wa Gerari, anatokewa na Mungu kwenye ndoto kumuonya amwache Sarah, aliyekuwa amemchukua ili awe mke wake bila kujua kuwa alikuwa mke wa mtumishi wa Mungu Abrahamu.

Huyu Mfalme Abimaleki ni mpagani wala sio mcha Mungu, lakini bado aliota anazungumza na Mungu!
Ndoto nyingine ni ya Yusufu aliota akiwa na miaka 17 akaonyeshwa maisha yake yatakavyo kuwa baadaye,na yote aliyo ota yakaja kutimia baada ya miaka 13,pamoja na kwamba alipitia changamoto nyingi sana.Ali hukumiwa kufa na kaka zake kwa sababu ya ndoto zake ,

Kaka zake wakatafuta njia  ya namna ya kumua , wakaona sio vizuri wao wamuue bali wa muuze ili akafie mbali ili ndoto zake zisitimie,Yusuf akauzwa kwa Waishumael ambao wakamleta mpaka MISRI alikouzwa kwenye nyumba ya mfalme akiwa nyumbani mwa Potifah mke wa mfalme alitaka kumbaka japo ni tukio la kipekee mwanamke kutaka kumbaka kijana,lakini kijana Yusufu alikuwa mwaminifu  kwa Mungu wake YEHOVA aliyemuonyesha maisha yake yajayo ,akakataa akisema siwezi kumtenda MUNGU dhambi kubwa namna hii.

Tukio hilo la kukataa kutenda dhambi lilimpelekea Yusufu kuingia kwenye changamoto ya tatu kwa kutiwa gerezani

Changamoto ya nne ni pale Yusufu aliposahauliwa na mnyweshaji wa mfalme,alimwahidi baada ya kutafsiriwa ndoto yake akasema sitakusahau nikifika kwa mfalme.
Ndugu yangu Mungu akikupa ndoto uwe tayari kukabiliana na changamoto nyingi kabla ndoto yako haijatimia.

Ndoto nyingine ni za wahudumu wa mfalmeFarao.     Mwanzo 40:1- wote wawili walitenda kosa moja,walihukumiwa pamoja,waliwekwa gereza moja wote wawili,waliota ndoto zenye jumbe zinazoelekeana na kazi zao kwa mfalme ,ndoto ya mmoja ilikuwa njema naya mwingine ilikuwa mbaya.

Hapa tunajifunza mgawanyo wa ndoto kuwa kuna ndoto mbaya, na kuna ndoto nzuri.
Mwota ndo mwingine ni mfalme Farao., Mwanzo 41:1- huyu tena alikuwa siyo mcha Mungu ndiyo maana hata alipoota ndoto aliwaita waganga na wachawi ili wamtafsirie ndoto yake, japo pia aliota ndoto ilotoka kwa Mungu ,na hii ndiyo ndoto iliyotimiza na kudhihirisha ndoto aliyoota Yusufu miaka 13 iliyopita.

SASA:
Ukiziangalia ndoto zote hizi unaziona zina ujumbe wa Mungu moja kwa moja,na kila ndoto kwenye Biblia ilikuwa ya kweli na ikatimia sawasawa na ilivyootwa.
Ndugu zangu tukisoma kwenye Biblia tunaona nabii Yoeli alionyeshwa juu ya kizazi chetu kuota ndoto.

YOELI 2:28. Hata itakuwa baada ya hayo ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya  wote wenye mwil, wana wenu waume kwa wake watatabiri, wazee wenu wataota ndoto na vijana wenu wataona maono.
Hapo Yoeli anaona wana wa kike na wa kiume wanatabiri,wazee wanaota ndoto na vijana wanaona maono.Tunaweza kujiuliza je unabii wa Yoeli umeshaanza kutenda kazi?  Jibu ni ndiyo .
Matendo2:16-17;  lakini jambo ni lile lililonenwa kwa kinywa cha Nabii Yoeli, itakuwa siku za mwisho asema Mungu nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabir, na vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto!

Majeshi ya Bwana ikimsikiliza Baba kwa makini.
Kupitia maelezo hayo ya Petro akithibitisha kutimia kwa unabii wa Yoeli, tunapata picha  niwazi aliyotabiri Yoeli yanatendeka sasa katika kizazi chetu .Lakini pia kuna jambo la ajabu linaloaendelea duniani leo, Yoeli alitabiri ndoto zitaotwa na  ‘mtu amelala anaota anajamiahiana na mtu asiye mke wake au mume wake, mara mtu anaota anakabwa na JINAMIZI! Mara mtu anaota anakula manyama ya ajabu ajabu au vyakula, Ndoto za siku hizi nyingi zimejaa vitisho mtu anamka amekata tamaa kabisa au kavunjika moyo kabisa kwasababu tu ya ndoto alizo ota, ndoto nyingi siku siku hizi zimebeba jumbe za hatari kuliko kuleta matumaini. SASA TUJIULIZE JE!!?  Hizi ndoto za kuota mara unakabwa,mara unaota unafukuzwa na kambako jeusi je hizi ndizo ndoto alizoziona Yoeli?.
wazee baada ya MUNGU kumimina ROHO wake .Lakini kinyume chake siku hizi kila mtu anaota ndoto,kuanzia watoto wadogo mpaka wazee,na ndoto zenyewe ziko tofauti kabisa na zile ndoto tulizoziona kwenye Biblia ambazo zilikuwa na ujumbe wa MUNGU,bali za sasa ni za ajabu:


Baba akisisitiza Kanisa lazima liamke
ZEKARIA 10:2
‘’Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili ,nao waaguzi wamenena uongo;nao wameleta habari za ndoto za uongo,wafariji bure;kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo ,wateswa,kwa sababu hapana mchungaji.’’
Kupitia Zekaria tunaweza kuona chanzo cha ndoto za sasa ni kupitia vinyago  (ibada ya sanamu, na  mawakala wa shetani  waaguzi)     

KUNA SABABU KUU MBILI ZA MAWAKALA  WA SHETANI KULETA NDOTO ZA UONGO:
(a)    Kuwanajisi watu ili wapate  kuwatesa.
(b)   Kwa sababu hapana mchungaji sawasawa na zekaria alivyosema

Hii inamanisha kuwa kanisa limelala,watu wanakwenda kanisani kwa ajili ya kuimba tenzi na pambio, Jambo hilo siyo baya,lakini wachungaji tujue kanisa lipo kwa ajili ya kupambana na malango ya kuzimu.     MATHAYO 16:18; Namii nakwambia leo wewe ndiwe Petro na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa lango wala milango ya kuzimu haitakishinda.  Na kwa kuthibitisha kuwa kanisa lijijue kuwa lipo vitani wakati wote,Mtume P AULO  anaeleza aina ya vita vyetu  katika .Waefeso 6:12;  kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;  bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

 Napenda utambue kuwa tunapo jifunza habari za ndoto tunaongelea mambo ya rohoni . mwanadamu ameganyika vipande viwili mtu wa ndani (Inner man) na mtu wa nje yaani mwili (outer man) tusemeje sasa mwanadamu ninani? Mwanadumu ni roho yenye nafsi inayokaa ndani ya nyumba na hiyo nyumba inaitwa mwili. 2Korintho 12:2 Namjua mtu mmoja katika Kristo yapata sasa miaka kumi na minne (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa mpaka mbingu ya tatu.

 Hapa Paulo anajaribu kukumbuka miaka kumi na nne iliyopita siku alipotokewa na Bwana Yesu. Lakini pia kupitia Mtume Paulo tunathibitisha kuwa mtu anaweza kuwa ndani ya mwili na nje ya mwili. Jambo hutokea kwenye ndoto pia mtu amelala Moshi lakini anaweza kuota yuko Nairobi na akaona vitu vingi napengine nayeye akashiriki kwa namna moja au nyingine lakini mwisho wa siku anamka na ndipo anatambua kwamba kumbe ni ndoto tu! Sasa huko kwenye ulimwengu wa roho kwakuwa tumeona mtume Paulo akisema kuna Falme na mamlaka, wakuu wa giza na majeshi ya pepo wa baya hao ndiyo wanavuvia ndoto mbaya Duniani. Kwa watu walio na Yesu(waliokoka) ukitaka kuwa salama na kujitenganisha na ndoto mbaya nilazima uchukue hatua ya kuwasambaratisha  hawa maadui kwenye ulimwengu wa roho kwa kutumia jina la YESU!

NDUGU ZANGU : Huu siyo wakati wa kulia lia na kulalamika,huu ni wakati wa kuvaa silaha za MUNGU tayari kwa kumsambaratisha  shetani na mawakala zake wanaotuletea ndoto za ajabu ajabu,na pia tunayo damu ya YESU iliyomwagika msalabani kwa ajili yetu.
SASA:  Tuitumie damu hii kufuta ndoto zote za kishetani tulizoota, tunazozikumbuka na tusizo zikumbuka,tuzifute ndoto zote mbaya kwa damu ya mwanakondoo YESU KRISTO.

TUMIA JINA LA YESU KUWASAMBARATISHA  MASHETANI  WOTE  WASIMAMIZI  WA  NDOTO  MBAYA.

MWISHO; ZIITE  NDOTO ZAKO ZOTE  NZURI  ZA  KIMUNGU  ULIZOWAHI   KUOTA  ZITIMIE   KWENYE MAISHA YAKO  KWA JINA LA YESU,,SEMA NDOTO ZANGU NJOOOOOOOOOO  KWA  JINA  LA  YESU
                                              
                      AMINA  MUNGU  AKUBARIKI 
  
 KARIBU  UFUFUO  NA  UZIMA  MOSHI –KILIMANJARO   TANZANIA

Comments