YESU ALIFANYIKA LAANA KWA AJILI YETU


Wagalatia 3:13-14
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Kwa kupigwa kwake na hatimaye kusulubishwa msalabani alitukomboa kutoka katika:
1) Dhambi
Mathayo 26:28
kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
1Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
2) Magonjwa na udhaifu wote
Mathayo 8:14-17
Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo, akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na akayachukua magonjwa yetu.
Isaya 53:4-5
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
1Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
3) Umaskini
2Wakorintho 8:9
Maana nimejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Watu waliookolewa, hawako tena chini ya laana. Hivyo kama unavyozikataa na kuzipinga dhambi, vivyo hivyo inakupasa kuyakataa na kuyapinga magonjwa na udhaifu wote na kuukataa umaskini.
Pia kama bado haujamkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako (hujaokoka) saa ya wokovu ni sasa amua kumfuata Yesu ili uweze kuwekwa huru mbali na laana za shetani.

MUNGU akubariki sana .
By Nyandula Mwaijande.

Comments