ACHA MUNGU AITWE MUNGU: MUNGU AMUOKOA RAIA WA IRAN ALIYEBADILI DINI NA KUHUKUMIWA KUNYONGWA.

Pastor Youcef Nadarkhani akiwa na familia yake.
ACHA MUNGU AITWE MUNGU!
Kuachiliwa huru kwa mtumishi huyu ulikuwa ni Muujiza Mkubwa. 

Ni Pastor Youcef Nadarkhani mzaliwa wa Irani, alikamatwa mwishoni mwa mwaka 2010, na kuhukumiwa kifo kwa kosa la kuacha uislamu na Kumuamini Yesu.

Alidumu gerezani kwa muda wa miaka mitatu, ilipokaribia siku ya kunyongwa, watesi walimpa mateso na vitisho vya hali ya juu wakimlazimisha aikane Imani yake lakini hakutetereka.
Watesi walipoona Imani yake ni thabiti, wakaja na gia ya kumbembeleza ili angalau atamke neno moja tu la kumkana Yesu na amkiri shetani! Alidumu kuwa Mwaminifu, siku ya kunyongwa kwake ilipofika Yesu alijidhihirisha Mwenyewe, mipango ya shetani ikabatilishwa.


Zingatia: Atakaye kuiokoa nafsi yake ataipoteza, na atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili ya YESU KRISTO  ataiokoa (Mathayo 25)





.

Comments